Majaliwa aliyasema hayo Dar es Salaam jana kwenye kongomano baina ya ujumbe wa Tanzania na Rais wa Vietnam, Truong Tan San aliyeongozana na ujumbe wake katika ziara ya siku nne nchini na wafanyabiashara wa Tanzania.
Waziri Majaliwa alisema Tanzania ni nchi yenye mazingira mazuri ya uwekezaji katika nyanja mbalimbali na kusisitiza kwamba wanaotaka kuwekeza nchini wanafurahia mazingira hayo na uwepo wa dhamana ya mitaji waliyowekeza.
“Ukiwekeza Tanzania una uhakika wa usalama wa mtaji na uwekezaji wako kwa sababu nchi imesaini mikataba mbalimbali ya kupinga utaifishaji mali za wawekezaji na kuhimiza uwekezaji wa kigeni katika mazingira salama na yenye amani,” alisema Majaliwa.
Alisema kila mara nchi imekuwa ikiboresha sheria na kuimarisha ushirikishwaji wa sekta binafsi ili kuchochea mazingira ya uwekezaji kwa lengo la kuimarisha uchumi na kuinua maisha ya wananchi wake.
Akizungumzia soko mara baada ya kuwekeza nchini, Waziri Majaliwa alisema, wawekezaji wanaowekeza nchini wana uhakika wa masoko ya zaidi ya watu milioni 300 waishio Mashariki na Kusini mwa Afrika, ambao hufurahia kuwepo kwa nchi katika Jumuiya kama ya SADC na EAC.
Aidha, nchi zaidi ya sita ambazo hazina bahari hutegemea bandari ya Tanzania kufanya biashara na masoko katika eneo hilo. Akizungumzia uwekezaji kutoka nje ya nchi, Waziri Majaliwa alisema serikali imekua ikiboresha mazingira ya uwekezaji na hiyo imeongeza uwekezaji kutoka nje.
Alisema mfano mzuri ni uwekezaji wa Kampuni ya Viettel Tanzania Ltd, ambao ni wawekezaji kutoka Vietnam
No comments:
Post a Comment