ZAIDI ya wasichana 100 wa ngazi mbalimbali za elimu wakiwemo wanaosoma elimu ya juu wilayani Siha, mkoani Kilimanjaro, wamepatiwa ufadhili wa masomo kama njia ya kuwezesha mtoto wa kike kukabiliana na changamoto ya maisha
Mbunge wa jimbo hilo, Dk Godwin Mollel alisema ufadhili kwa wanafunzi hao ulianza kutolewa kabla ya yeye kuwa mbunge wa jimbo la Siha.
Alisema lengo ni kuhakikisha mpango huo wa ufadhili unakuwa endelevu ili kuona kwamba wasichana wengi zaidi wananufaika elimu ambayo ndiyo mkombozi wao.
“Katika wanafunzi hao, wawili wapo ngazi ya diploma na wengine ngazi tofauti, hii itawapa fursa hapo baadaye kumudu maisha kwa kukuza uchumi….hata hili la uzazi wa mpango na mengine yote yanayohusu uzazi na malezi kwa watoto watalimudu, na taifa litapiga hatua za maendeleo,” alisema.
Dk Mollel alisema elimu kwa wasichana itasaidia kupunguza idadi ya vifo vya wajawazito na watoto chini ya miaka mitano, jambo ambalo litasaidia kupunguza idadi ya kitaifa ya vifo vya wanawake 7,900 kila mwaka.
“Mimi njia kubwa ambayo nitaipa nafasi ni elimu, hili suala la lishe kwa wajawazito halitakuwa taabu kupatikana, ukimpa elimu mwanamke hata chakula kinachostahili kwa ajili ya mjamzito na mtoto aliyeko tumboni kitakuwa ni kile chenye manufaa na siyo kujaza
No comments:
Post a Comment