Monday, 7 March 2016

UJINGA ULEULE WA UWANJA WA TAIFA, SAFARI HII ULIKUWA PALE WHITE HART LANE



Si unajua namna ambavyo mashabiki wa Simba na Yanga wanavyofanya vurugu na wakati mwingine kuumizana inapofikia mechi kati ya timu hizo!

Ninaamini umekwua ukiona wadau wenye akili timamu wanavyopinga vurugu hizo na kusisitiza soka ni starehe lakini wako ambao hawasikii!

Sasa mambo hayo yalitokea juzi kwenye Uwanja wa White Hart Lane wakati Tottenham walipowakaribisha watani wao wakubwa, Arsenal.

Pambano hilo linajulikana kama North London Derby na ilikuwa si mchezo ndani ya uwanja lakini mashabiki wakatandikana hadi kutoana damu.

Mechi iliishia kwa sare ya mabao 2-2 na askari polisi walilazimika kufanya kazi ya ziada kuwatawanya mashabiki hao.



No comments:

Post a Comment