Mkwasa amewarejesha kikosini kipa Shaaban Kado na kiungo Mwinyi Kazimoto, huku akiwatema nyota wa Yanga, beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na winga Simon Msuva. Amemtema pia kiungo mshambuliaji Mrisho Ngassa anayecheza soka ya kulipwa Afrika Kusini katika klabu ya Free State Stars.
Akizungumza jana Dar es Salaam, Mkwasa amewaomba wachezaji aliowaita kujiweka fiti kuanzia kwenye mazoezi ya klabu, kwani hakutakuwa na muda wa kufanya mazoezi ya muda mrefu ya pamoja.
Timu hizo zitachuana Machi 23 mjini ND’jamena, Chad na kurudiana siku nne baadaye jijini Dar es Salaam. “Ligi Kuu ya Vodacom, michuano ya klabu Afrika, inachezwa wikiendi ya tarehe Machi 18-20, hivyo wachezaji wote watakuwa na majukumu katika timu zao, muda wa kufanya
No comments:
Post a Comment