Alitua kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza saa 11:40 jioni na kupokewa na viongozi mbalimbali, wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo.
Baadaye alikagua vikundi vitatu vya ngoma.
Aidha mamia ya wananchi walijipanga kwenye barabara ya Airport, kumlaki Waziri Mkuu huku baadhi yao wakiwa na mabango yenye ujumbe tofauti kwenda mjini kumlaki.
Hii ni mara ya kwanza kwa waziri huyo kutua Kanda ya Ziwa tangu ateuliwe kuwa Waziri Mkuu wa 11 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Waziri Mkuu ataanza ziara mkoani Simiyu, akianzia wilayani Busega. Atakapomaliza ziara hiyo mkoani Simiyu ataenda mkoani Kagera na Geita kwa muda wa siku 14.
No comments:
Post a Comment