Friday, 11 March 2016

Vijiji 356 vya Sengerema kuunganishiwa umeme




Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.

 
VIJIJI 356 wilayani Sengerema vitaunganishiwa umeme baada ya kuingizwa kwenye awamu ya pili ya mradi wa Wakala wa Usambazaji Umeme Vijijini (REA), imeelezwa.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani alisema hivyo jana wakati akizungumza na wakazi wa Bondo wilayani humo alipofanya ziara kukagua miradi ya umeme iliyo chini ya wakala huo.

Alisema, Serikali imejipanga kuhakikisha wananchi katika maeneo hayo wanapata umeme wa uhakika. “Vijiji 356 vitaunganishiwa umeme kupitia REA, kazi yetu ni kuwapatia huduma hiyo na wananchi wanapaswa kujua kuwa atakayekataa kuutumia wakati ameunganishiwa atafikishwa mahakamani,” Dk Kalemani alisema na kusababisha waliokuwa wakimsikiliza kufurahi kwa vicheko.

Aliwataka viongozi wa kata hiyo na Halmashauri kuhakikisha wanatumia fedha za mapato kutatua matatizo ikiwemo uhaba wa madawati. “Suala la madawati sio lazima mlipeleke Serikali Kuu, liko ndani ya uwezo wenu hivyo msilifanyie mzaha. Kila mtu anapaswa kushiriki kutoa mchango wa hali na mali,” alisema.

No comments:

Post a Comment