Alitoa pongezi hizo jana wilayani humo, alipozungumza na wanahabari kuhusu utekelezaji wa ahadi za Rais alizozitoa wakati wa kampeni ya Uchaguzi Mkuu. Alisema, Rais ametoa Sh milioni 700 zitakazotumiwa na Mkandarasi Mshauri kufanya upembuzi yakinifu kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo, ambalo kwa mujibu wake litakuwa ni la kwanza na la aina yake kuwahi kujengwa kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.
“ Kwa niaba ya wananchi wa Sengerema nachukua fursa hii kumpongeza kwa dhati Rais wetu kwa kuanza kutekeleza moja ya ahadi muhimu aliyowaahidi wananchi wa Sengerema ya ujenzi wa daraja la kisasa kwenye kivuko cha Kigongo- Busisi,” Ngeleja alisema.
Alisema, Serikali imekwishatangaza zabuni ya kuanza kufanya upembuzi yakinifu kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo, jambo lililowapa faraja wakazi wa Sengerema na mikoa ya jirani. Alisema, daraja hilo litakapokamilika litaharakisha shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na kusaidia kukuza uchumi wa wananchi na kuondokana na umasikini wa kipato.
No comments:
Post a Comment