Tuesday, 1 March 2016

UJASIRIAMALI HAI













Mkufunzi wa somo la Online Journalism Mwl Elihuruma Chao akiwaelekeza wanafunzi wa darasa la AICC katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha















 Mkufunzi Chao ndani ya darasa la AICC



















Mkufunzi Chao akiwa ofisini kwake katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha



Mkufunzi  wa kitengo cha uzalishaji wa vipindi na Mwl wa somo la uandishi wa habari za mtandaoni Bw. Elihuruma Chao amewaasa wanafunzi wa darasa a AICC katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha  kupenda kuperuzi  blog zao na kuweka habari na matukio mbalimbali.

 Ameyasema hayo leo wakati akifundisha somo hilo darasani na kuwaahusia wanafunzi hao kuperuzi blog zao kwani wanaweza tapata pesa kwa njia ya matangazo kutoka kwa wadhamini mbalimbali
Pia amesema wanafunzi wamekuwa wazembe kuperuzi blog zao na kuwezakupoteza  watembeleaji (viewers ) wa blog zao 

“Watu wengi wanaishi kutokana na blog kwani imekuwab ni kama ajira kwa sababu wanapata matangazo kutoka kwenye makampuni mbalimbali na kuweza kujipati a mahitaji yao ya kila siku”Alisema Mwl Chao

Licha ya kusema hayo wanafunzi waliweza kujitetea kuwa wamekuwa na  uhaba wa vifaa vya utendeaji kazi  kama vile Laptop,camera pamoja na pesa ambazo zinatumika kwa  nauli pindi wanapotaka kwenda kuchukua habari na kununulllia vocha za kuwasaidia kuperuzi mitandaoni














No comments:

Post a Comment