Showing posts with label Habari Kitaifa. Show all posts
Showing posts with label Habari Kitaifa. Show all posts

Wednesday, 5 April 2017

vifo vya ng'ombe vyaleta mtafaruku


















JUMLA ya ng’ombe 22 wamekufa ghafla wakiwa wanachungwa katika kitongoji cha Kirumi Kijiji cha Tairo, Bunda mkoani Mara na kuleta hofu kubwa kwa wananchi wa maeneo hayo.
Kwa mujibu wa Ofisa Mifugo na Uvuvi katika Halmashauri ya Mji wa Bunda, Rick Kaduri, tukio hilo limetokea Aprili 3 saa tisa mchana katika kitongoji hicho wakati ng’ombe hao wakichungwa na watoto wadogo.
Kaduri alisema ng’ombe waliokufa ni mali Mwita Masero mkazi wa kijiji cha Tairo katika Halmashauri ya Mji wa Bunda na thamani yake ni zaidi ya Sh milioni tisa.
Alisema uchunguzi wa awali unaonesha kuwa mifugo hiyo imekufa kutokana na kula majani ambayo kiuhalisia huwa yana sumu kali, ambapo mifugo ikiyala kwa wingi hasa yanapoanza kuota upata madhara ya mfumo wa chakula tumboni na hatimaye kufa.
Aidha, Kaduri alitoa mwito kwa wananchi kufukia mizoga ya mifugo hiyo na kutokuthubutu kujaribu kula nyama ya ng’ombe wanaokufa ghafla.
Hata hivyo, alisema wamechukua sapuri ya vipimo ambavyo vitapelekwa kwa wataalamu wa mifugo na kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa uchunguzi zaidi juu ya vifo vya ng’ombe hao.

Saturday, 4 February 2017

Makubwa zaidi yaibuka dawa za kulevya




SIKU moja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutangaza vita dhidi ya watu wanaojihusisha na dawa za kulevya, makubwa zaidi yamezidi kujitokeza baada ya orodha ya watu hao wanaojihusisha na biashara hiyo haramu kuongezeka.
Mkuu huyo wa mkoa amemuagiza Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro kuwaongeza askari wengine watatu katika orodha ya watuhumiwa hao ambao alidai katika wiki mbili zilizopita walipewa Sh bilioni moja kutokana na biashara hiyo.
Aliwataja askari hao kuwa ni Muddy Zungu, Fadhili na Ben huku wengine wanaopaswa kuongezwa katika orodha hiyo ni pamoja na msanii Vanesa Mdee na Video Queen, Tunda Sebastian.
Aidha, Makonda alimuagiza Sirro kuhakikisha wasanii na watu wengine walioko kwenye orodha aliyoitaja awali ambao hawakufika, wakamatwe mara moja na wawekwe ndani hadi Jumatatu kwa ajili ya mahojiano.
“Hawa nataka waunganishwe na wale wenzao, hatuwezi kuwa na watumishi wanaochafua taaswira ya jeshi la polisi na nimepata taarifa mmoja amenunua nyumba Kigamboni,” alisema Makonda.
Makonda pia alimtaja mtu mwingine ambaye ni mfanyabiashara mkubwa wa dawa hizo, Omari Sanga kuwa ni mmoja kati wa watu waliosababisha asilimia 65 hadi 70 ya Watanzania waishie kwenye jela nchini China.
Pia aliitaja hoteli ya Meditteranian iliyopo Kawe kuwa nayo ni miongoni mwa hoteli ambazo zimekuwa zikifanya biashara hiyo kinyume na leseni waliyopewa.
Watuhumiwa waliofika ni pamoja na aliyewahi kuwa Miss Tanzania, Wema Sepetu, Khaleed Mohammed (TID), Hamidu Chambuso (Dogo Hamidu/ Nyandu Tozzy) pamoja na Babuu wa Kitaa.

Monday, 25 July 2016

Rais Magufuli mgeni rasmi Sherehe za Mashujaa Dodoma



AMIRI Jeshi Mkuu, Rais John Magufuli atakuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa Kitaifa, yatakayofanyika mjini Dodoma leo.

Hiyo itakuwa ni mara ya kwanza kwa maadhimisho hayo kufanyika nje ya Jiji la Dar es Salaam, tangu Tanzania ipate Uhuru wake mwaka 1961. 

Pia, itakuwa ni mara ya kwanza kwa Rais Magufuli kuongoza maadhimisho hayo tangu alipochaguliwa Oktoba mwaka jana.

"Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yatafanyika kitaifa mkoani Dodoma katika Uwanja wa Mashujaa siku ya Jumatatu (leo) Julai 25, 2016 kuanzia saa 1 kamili asubuhi hadi saa 4:30 asubuhi. 

“Mgeni rasmi atakuwa Rais John Magufuli," alisema Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana, kwenye mkutano wake na waandishi wa habari, jana.

Alisema anaishukuru serikali kwa kuupatia mkoa huo, ambao ni Makao Makuu ya nchi, heshima ya kipekee katika historia ya nchi ya kuwa mwenyeji wa maadhimisho hayo kitaifa.

Rugimbana alitaja shughuli zitakazofanyika siku hiyo kuwa ni gwaride la maombolezo litakaloshirikisha vikosi vya majeshi ya ulinzi na usalama vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Polisi na Magereza.

Kutakuwa pia na upigaji mizinga na uwekaji wa silaha za asili na shada la maua kwenye mnara, kama ishara ya kumbukumbu kwa mashujaa. Shughuli nyingine ni utoaji wa dua na sala, utakaofanywa na viongozi wa madhehebu ya dini.

Rugimbana aliwataka wakazi wa Dodoma kujitokeza kwa wingi siku hiyo kwenye Viwanja vya Mashujaa kushiriki kwenye maadhimisho hayo. Alisema hadi jana, maandalizi yote muhimu kwa ajili ya shughuli hiyo yalikuwa yamekamilika.

Thursday, 2 June 2016

Maswali na majibu katika kikao cha bunge


 
 Kikao cha bunge la wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari kilichowakutanisha baadhi mawaziri
kutoka wizara tofauti tofauti kwa lengo la kuwasilisha ripoti na kujibu maswali ya wabunge hao.

Wizara ambazo zilitakiwa kuwasilisha ripoti zao ni wizara ya Habari,fedha,wizara ya sheria na maadili pamoja na wizara ya afya ulinzi na makazi.Kutokana na wingi wa maswali mengi kwa wizara ya habari  hivyo kupelekea wizara nyingine kutowasilisha ripoti                                                            




 

 
Spika wa bunge Mh Gabriel(kushoto) akiwa na katibu wa bunge Mh Elizabeth Gabriel


















Mh Elia Baraka naibu waziri wa Elimu akijibu maswali yaliyoulizwa na wabunge



















Mawaziri na manaibu waziri wa wizara mbalimbali wakisubiri kutumbuliwa na wabunge

Tuesday, 31 May 2016

Majambazi wauawa wakikimbizwa na polisi

Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam, Simon Sirro

WATU wawili wanaosadikiwa kuwa ni majambazi, wameuawa na mwingine mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kujihusisha na ujambazi jijini Dar es Salaam.

Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam, Simon Sirro wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Alisema tukio hilo lilitokea Mei 28 mwaka huu baada ya polisi kupata taarifa kuwa maeneo ya Mburahati kuna majambazi watatu, ambao walikuwa wanafukuzwa na kundi la bodaboda huku wakifyatua risasi.

Sirro alisema katika ufuatiliaji askari walifika katika eneo hilo na kukuta jambazi mmoja akishambuliwa na wananchi baada ya silaha aliyokuwa akiitumia kuishiwa risasi.

Jambazi huyo alikutwa na silaha moja, bastola LLA yenye namba 649440. Alisema majambazi wengine wawili, walikimbia wakiwa na bodaboda yenye namba za usajili MC 444 BFY.

Polisi waliwakimbiza wakishirikiana na madereva bodaboda hadi kufika katika eneo la Kisukuru, ambako majambazi hao walianguka na kuangusha bastola yao aina ya Chinese Star, ndipo wananchi walianza kuwashambulia kwa mawe na fimbo.

Aliongeza kuwa majambazi hao, walishambuliwa baada ya muda mfupi walifariki dunia huku mwingine alifanikiwa kukimbia na begi dogo jeusi lililokuwa na fedha.

Sirro alisema awali majambazi hao, walikuwa watatu wakiwa kwenye pikipiki maeneo ya Buguruni, ambapo walifanya tukio la uporaji wa Sh 500,000 mali ya Mushi Bakari, aliyekuwa na gari namba T 786 CZI Toyota IST ambaye walimjeruhi mkono wa kulia.

Katika tukio jingine, jeshi hilo limefanikiwa kumkamata mtu mmoja anayetuhumiwa kuwa jambazi huko Temeke akiwa na bastola Glock P241 yenye namba NK 172374 ikiwa na risasi 14 ndani ya magazini.
Alisema jambazi huyo alikamatwa baada ya kufanya tukio la uporaji maeneo ya Chang’ombe Maduka Mawili ya Tigo Pesa akiwa na mwenzake, ambapo walikimbia kwa kutumia pikipiki.

Monday, 30 May 2016

Rais Magufuli amteua Mama Makinda kuwa Mwenyekiti Bodi ya NHIF, Jaji Lila kuwa jaji Mahakama ya Rufani

























Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Mhe. Jaji Shabani Ally Lila kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.

Kabla ya uteuzi huo Mhe. Jaji Shabani Lila alikuwa Jaji Kiongozi. Uteuzi huu umeanza leo tarehe 30 Mei, 2016.

Wakati huo huo, Rais Dkt. Magufuli amemteua Mhe. Anne Semamba Makinda kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF). Uteuzi wa Mhe. Anne Semamba Makinda ambaye ni Spika Mstaafu wa Bunge Ia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umeanza tarehe 25 Mei, 2016.

Mhe. Anne Semamba Makinda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Ali Mchumo. Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemteua Prof. Apollinaria Elikana Pereka kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (Dar es salaam Institute of Technology -DIT).

Prof. Apollinaria Elikana Pereka ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Morogoro. Prof. Pereka anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Fredrick Mwanuzi ambaye amemaliza muda wake. Uteuzi huu umeanza leo tarehe 30 Mei, 2016.

Saturday, 28 May 2016

Majaliwa asafiri kwa mabasi ya haraka



WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amekagua utendaji kazi kwenye mabasi yaendayo haraka yanayotoa huduma katika Jiji la Dar es Salaam na kubaini changamoto kadhaa, ambazo amesema zitarekebishwa kadri mradi unavyoendelea.

Waziri Mkuu ambaye alilipa nauli na kupanda basi namba 23 lenye usajili namba T125 DGW kuanzia kituo cha Ferry, Kivukoni, ametumia muda wa dakika 50 kufika Kimara Mwisho kwa usafiri huo. Alipanda basi hilo saa 3:30 asubuhi jana na lilianza safari saa 3:33 baada ya kusubiri wengine wapande. Kwa wastani lilitumia kati ya dakika mbili hadi tatu kutoka kituo kimoja hadi kingine.

Basi hilo liliwasili Kimara Mwisho saa 4:23 asubuhi. Akizungumza na waandishi wa habari akiwa Kimara Mwisho baada ya kumaliza ziara hiyo fupi ya ukaguzi jana, Waziri Mkuu alisema aliamua kufanya ziara hiyo ya ghafla ili kuangalia matumizi ya njia za mabasi yakoje na kuona abiria wanaelewa vizuri namna ya kuitumia huduma hiyo.

Alisema ameridhishwa na mradi unavyofanya kazi, ila ameelezwa kuna usumbufu kwenye mageti wakati abiria wanapotaka kuthibitisha tiketi zao hasa wakati wa asubuhi kunapokuwa na msongamano wa abiria. Pia alielezwa kwamba kuna baadhi ya abiria wanakuja na tiketi za jana yake, jambo linaloleta usumbufu kwa sababu hazitambuliki kwenye mfumo wao.

“Nimeridhishwa na uharaka wa njia kwa sababu na mimi mwenyewe nimetumia dakika 50 kufika hapa ingawa kuna maeneo nimeona kuna haja ya kuwa na taa maalumu za kuzuia magari (special sensors) wakati mabasi yakipita ili kuepusha ajali,” alisema.

Aliyataja maeneo hayo kuwa ni kwenye makutano ya barabara za Morogoro na Mtaa wa Samora, Morogoro na Jamhuri na makutano ya Morogoro na Kisutu. Waziri Mkuu aliwataka Watanzania waende na tiketi rasmi badala ya kutumia tiketi za jana kwa sababu kufanya hivyo ni makosa na mtu anakuwa amedhamiria. “Hawa watachukuliwa hatua za kinidhamu.

Mtu akija na tiketi ya jana akamatwe na kupelekwa Polisi, huyu atakuwa amedhamiria,” alisema Waziri Mkuu wakati akizungumza na mhudumu mmoja katika kituo cha Kimara Mwisho.

 “Ninawasihi wananchi wanaotumia usafiri huu wajifunze kufuata utaratibu na kuwasisitizia kuwa kila abiria aje na tiketi ambayo ni rasmi,” alisema na kuongeza: “Haya mabasi nimebaini yako vizuri.
Ninatoa msukumo kwa watumishi wa umma wapande mabasi haya ili kupunguza msongamano wa magari barabarani.” Katika kupunguza baadhi ya changamoto, Waziri Mkuu alisema Serikali itasimamia uboreshaji wa ukataji tiketi ili kuondoa usumbufu kwa abiria.

Pia alivionya vyombo vya moto viache kutumia njia maalumu ya mabasi hayo. Pia aliwataka Polisi wanaofanya doria za usiku kupita kwenye barabara za juu za abiria na kuwaondoa watu wanaolala kwenye maeneo kwani wanahatarisha usalama wa watu wanaotumia njia hizo. “Zile siyo sehemu za kulala, wanaofanya hivyo wanahatarisha usalama wa watumiaji wa njia hizo, kwa hiyo polisi wakiwakuta watu wa aina hiyo wawakamate mara moja,” alisema.

Kwa upande wake, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mohammed Mpinga ambaye alifuatana na Waziri Mkuu katika ziara hiyo, alisema amepiga marufuku magari na pikipiki kutumia njia hiyo hata kama ni magari ya Serikali.

“Tulishapiga marufuku magari na pikipiki kutumia njia hiyo hata kama ni magari ya Serikali, ninawasihi madereva watambue hili na watii,” alisema. Machi 22, mwaka huu, Waziri Mkuu alitembelea soko la Feri kwa lengo la kuangalia mfumo wa majiko ya gesi sokoni hapo (kuzuia moshi) na kukagua ujenzi wa ukuta unaotenganisha soko hilo na mabasi yaendayo haraka.

Aprili 15, mwaka huu, Waziri Mkuu alifanya kikao na kuwaagiza wakuu wa taasisi zinazohusika na utekelezaji wa mradi huo kuhakikisha wanatoa elimu kwa umma ili kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza pindi majaribio yakianza.

MKUU WA MKOA AFUNANIWA AKIFANYA MAPENZI NA MWANAYE, TAZAMA VIDEO HAPA.

Mkuu wa zamani wa Mkoa wa Kaskazini Pemba na mshauri wa Rais wa Zanzibar kisiwani humo, Dadi Faki Dadi amekamatwa akituhumiwa kufanya mapenzi na mtoto wake wa kambo.

Dadi alikamatwa juzi akidaiwa kukutwa na mtoto huyo wa mkewe wa ndoa mwenye umri wa miaka 21 katika nyumba ya kulala wageni inayoitwa Executive, jirani na makao makuu ya Uhamiaji Zanzibar katika eneo la Kilimani chini na Maisara, mjini Unguja.

Mwanasiasa huyo alijikuta akipigwa pingu na polisi akiwa kifua wazi mbele ya mkewe na wanafamilia na kisha kupelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Mwembemadema.

Picha za video zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, zilimwonyesha Dadi akikabiliwa na mashambulizi makali ya maneno kutoka kwa watu waliomkamata, akiwamo mkewe.

“Mwacheni avae nguo kwanza, mpeleke bwana, twende bwana..." ni baadhi ya maneno yanayosikika katika video iliyorekodiwa wakati wa kumtia mbaroni.

Taarifa zilizopatikana miongoni mwa wanafamilia ya kiongozi huyo, zilidai kwamba alikamatwa baada ya kumtilia shaka binti huyo kutokana na mienendo yake ya hivi karibuni na kuamua kumfuatilia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam alithibitisha kumshikilia Dadi kwa muda kabla ya kumwachia kwa dhamana.

“Kijamii alitenda kosa, lakini sisi tunaendelea kufanya uchunguzi, iwapo tutabaini ametenda kosa la kisheria na anaweza kuwa mashtaka tutamkamata ili kumpeleka katika vyombo vya sheria,” alisema Mkadam.

Mmoja wa wanafamilia ambaye aliomba jina lake lisitajwe alisema: “Mwizi siku zake ni arobaini, tulimtega na hatimaye tumemnasa sasa tuone mwisho wake utakuwa nini na kipi kitajiri baadaye.”

Friday, 27 May 2016

Hatimaye washindi wa bonanza la utangazaji katika chuo cha A.J.T.Cwamepatikana


Darasa la Mbuga ya Ngorongoro katika chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha(Ajtc) wakishangilia mara baada
ya kuibuka washindi katika michano ya utangazaji iliyofanyika chuoni hapo.

Michuano ya utangazaji katika chuo cha uandishi wa habari na utangaza Arusha
 (A.J.T.C) imemalizika hii leo ambapo mshindi wa kwanza hadi wa mwisho amejulikana.

Darasa lililoibuka kidedea katika mashindano hayo yaliyochukua takribani siku tano linatambulika kwa jina la Mbuga ya Ngorongorongoro.

Mashindano hayo aliyohusisha madasa 13, darasa la Ngorongoro limejishindia kombe lenye thamani ya Tsh 10,000 pamoja na pesa taslimu Tsh 150,000.
Nafasi ya pili katika michuano hiyo Utangazaji ilichukuliwa na darasa linaloitwa Mlima Kilimanjaro huku wakijinyakulia tsh10,000 na darasa la Serengeti limeshikili nafsi ya tatu na kupewa zawdi fedha taslimu Tsh 75,000.
Mkurugenzi wa chuo hicho cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha bw Joseph Mayagila amewapongeza wanafunzi wote walioshiriki na kuwataka waendelee kujituma katika masomo yao ili wafanye vizuri katika tasnia ya uandishi wa habari na utangazaji.

Monday, 23 May 2016

‘Hakuna sababu kupima wabunge ulevi’










BAADA ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga kuingia bungeni akiwa amelewa, Ofisi ya Bunge imesema hakuna kanuni inayotaka wabunge wapimwe ulevi na haioni sababu ya kuwapima kwa sababu ni watu wazima.
Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel alisema, Kanuni za Kudumu za Bunge hazina kanuni inayozungumzia suala la ulevi. Akizungumza na gazeti hili, Joel alisema lakini katika mabunge mbalimbali duniani wameweka taratibu za kimaadili zinazowaongoza wabunge.
“Kwa kweli hakuna sababu ya kupima wabunge ulevi kwa sababu hawa ni watu wazima wanaojitambua. Kanuni za Bunge hazina kipengele kinachozungumzia suala la ulevi. “Lakini wabunge wanaandaa kanuni zao za maadili, humo ndio wataweka mambo yao ya nini cha kuzungumzwa na wabunge, kusema wenzao na mengineyo.
Ni Code of Conduct kwa wabunge wenyewe,” alisema Joel. Alisema hilo linafanyika katika mabunge mbalimbali duniani kwa kuwa na taratibu zao za kimaadili zinazowaongoza. Kaimu Katibu wa Bunge alisema hayo, baada ya kuulizwa na gazeti hili kuhusu hoja iliyoibuka baada ya kutenguliwa kwa uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kitwanga kwa kuingia na kujibu swali bungeni akiwa amelewa.
Kurugenzi ya Mawasiliano, Ikulu alisema Rais Magufuli alitengua uteuzi huo kutokana na kitendo cha Kitwanga kuingia bungeni na kujibu swali linaloihusu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi akiwa amelewa.
Hoja ya kutaka kuwapo kwa kipimo cha ulevi kwa wabunge kabla ya kuingia bungeni, ilitanda katika mijadala nchini juzi baada ya Kitwanga kufukuzwa. Mbunge wa Arusha Mjini, Gobless Lema ambaye pia ni Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ni mmoja wa waliounga mkono hoja hiyo.
Lema alikaririwa akisema katika taarifa ya habari ya kituo cha televisheni cha ITV juzi usiku, akipendekeza sasa kuwapo kwa kipimo cha ulevi kwa wabunge kabla ya kuingia ukumbini, akisema kitasaidia kuondoa wabunge na mawaziri walevi.
Katika taarifa yake saa chache baada ya kutimuliwa Kitwanga, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alisema uamuzi uliofanywa na Dk Magufuli umefuata kanuni za utumishi wa umma ambao unakataza mtumishi kulewa akiwa kazini.
“Zipo sheria za utumishi ambazo mtumishi hatakiwi kunywa pombe na wala hapaswi kulewa akiwa kazini… mtumishi anapaswa kuwa na akili timamu inayokuwezesha kufanya kazi za serikali,” alisema Majaliwa akijibu swali la mwandishi wa TBC1 aliyetaka kujua ukweli wa taarifa za kutimuliwa Kitwanga.
“Ni kweli Mheshimiwa Rais, Dk John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Charles Kitwanga kuanzia leo tarehe 20 Mei, 2016 baada ya kuonekana amelewa wakati wa kazi. Na hili lilibainika pale alipokuwa akijibu maswali ya wizara yake leo asubuhi,” alisema Waziri Mkuu.
Kwa utaratibu wa sasa, wabunge na wageni wote wanaoingia ndani ya viwanja vya Bunge, hukaguliwa kwa mashine maalumu, ambazo huangalia kama mtu amebeba vitu visivyokubalika, kama silaha, visu na vingine vyenye ncha kali.

Tuhuma za ubadhirifu fedha za uchaguzi zatua Takukuru









TUHUMA za ubadhirifu wa Sh bilioni 1.4 za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka jana, zilizotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa Halmashauri ya wilaya Mbinga mkoani Ruvuma, zimefikishwa kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Senyi Ngaga, alisema Takukuru inakamilisha uchunguzi wa kina ili wahusika waliofanya ubadhirifu huo wachukuliwe hatua za kisheria. Alisema hayo juzi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Alisema upo ukiukwaji mkubwa wa taratibu za manunuzi uliofanywa na wahusika waliopewa dhamana ya kusimamia matumizi yake. Ngaga alisema, ofisi yake baada ya kuunda tume ndogo na kubaini hilo, uchunguzi wa awali unaonesha Sh milioni 513 zimefanyiwa ubadhirifu .
Alisema, aliona ni vyema achukue hatua ya kukabidhi tuhuma hizo kwa Takukuru wafanye uchunguzi wa kina kutambua ni nani aliyehusika na ubadhirifu huo. Alisema, taarifa na majina ya wahusika waliofanya hivyo itatolewa baadaye Takukuru ikikamilisha kazi yake.
“Takukuru inaendelea na uchunguzi, ikikamilisha taarifa itatolewa. Katika maelezo yangu ya awali kwenye Baraza la Madiwani lililokaa juzi sikuhukumu mtu wala kusema amehusika, hivyo tusubiri tutajulishwa,” alisema.
Aliongeza kuwa, uchunguzi huo utakapokamilika, taarifa husika zitapelekwa kwa Mwenyekiti wa Baraza la Ulinzi na Usalama mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu awasilishe kwa Waziri mwenye dhamana. Awali, tuhuma za ubadhirifu huo, zilitolewa na Mkuu wa Wilaya kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa wilaya hiyo, Mei 11, mwaka huu.

Friday, 22 April 2016

semina ya ujasiriamali yafika tamati katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha ndani ya mwaka huu wa 2016















Mkufunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Bw. Massawe maarufu kwa jina la Kompyuta wizadi akifundisha njia mbalimbali za kutunza kumbukumbu za mapato ya biashara



Bw Massawe ameelezea njia tofauti tofauti ikiwa ni pamoja na kuwa na kitabu mbalimbali vya mapato ambavyo humsaidia mjasiriamali katika kufanya mahesabu ya biashara yake
























Wanafunzi wakifanya biashara katika ukumbi wa chuo hicho  baada ya kupata semina ya ujasiriamali




Makamo mkuu wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Ausha akifunga semina hii ya ujasiriamali iliyoanza tangu siku ya Jumatatu na kufikia kikomo siku ya leo



Kwa niaba ya mkurugenzi wa mafunzo katika chuo hicho Bw Elifuraha Samboto  ambaye ni makamo mkuu wa chuo ametangaza rasmi kufungwa kwa semina hiyo


Amewahasa wanafunzi kutokujiwekea dhana ya kutokuajiriwa pindi wamalizapo chuo kwani baadhi yao baada ya kupata semina hiyo wamekata tamaa ya kutokuajiriwa na kujiajiri wenywe

"Wengi wao wamesema hawataajiriwa na mtu yeyote pindi wamalizapo chuo, hilo wazo ni zuri ila lazima uwe na mtaji wa kujiajiri ,nawshauri  wanafunzi waajiriwe ili waweze pata mtaji pia kupata uzoefu wa mambo mbalimbali ya kibiashara"Alisema Bw. Samboto





Thursday, 21 April 2016

Je wajua mpango mkakati wa masoko?

Semina ya ujasiriamali imeendelea katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha  huku mada mbalimbali zikiwasilishwa na wakufunzi wa chuo hicho.

Muwasilisha  mada wa kwanza Bwana Thomas Majaliwa Ishengoma amesema biashara nyingi zinashindwa kudumu kutokana na ukosefu wa elimu muhimu katika biashara sanjari na kufanya biashara moja huku akiwashauri wajasiriamali na wanaohitaji kuwa wajasiriamali kuwa na mazoea ya kujaribu biashara zote.

Mkufunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Bwana Thomas Majaliwa Ishengoma akiwasilisha mada isemayo Ujasiriamali  katika semina ya ujasiriamali inayoendelea chuoni hapo.
Aidha amesema ili biashara idumu mjasiriamali anapaswa kufanya mambo ambayo yatainua biashara yake ikiwa ni pamoja na kutengeneza bidhaa yenye thamani kwa wateja sanjari na kuwa na nguvu ya kifedha.

Kwa upande wake mtoa mada wa pili Bwana Elifuraha Samboto ameelezea mambo muhimu ya mkakati wa kimasoko kuwa ni katika kuwalipa na kuwajali wafanyakazi, na kufanya utafiti wa kibiashara na kuwajali wateja.
Mkufunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Bwana Elifuraha Samboto akiwasilisha mada ya isemayo mkakati wa kukuza soko la biashara katika semina ya ujasiriamali inayoendelea chuoni hapo.
Hata hivyo amesema kuwa mjasiriamali ili aweze kuendelea na kufikia malengo yake anapaswa kuepukana na uvivu, wivu, Chuki, pamoja na hasira .

Naye mtoa mada wa tatu Bwana Elihuruma Chao ameelezea kanuni muhimu za mjasiriamali kuwa ni lazima aipende kazi anayofanya, uwezo wa kusimamia kazi, kuthubutu kufanya kile ambacho amekusudia pamoja na kuwa na nidhamu katika biashara anayoifanya.

Makamu mkuu  wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Bwana Elihuruma chao akiwasilisha mada ya isemayo maadili ya biashara katika semina ya ujasiriamali inayoendelea chuoni hapo.
Aidha amesema ili mjasiriamali aendelee mbele lazima afuate maadili ya biashara ambayo ni kuheshimu hadhi ya kila mfanyakazi, kuwa mwaminifu katika kutoa ahadi za kweli kwa wateja wake na kuendeleza mahusiano mazuri  kwa wateja wake.
Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha wakisikiliza pamoja na kuandi kakile kinachowasilishwa  na wakufunzi wa chuo hicho katika semina ujasiriamali inayoendelea chuoni hapo.
Semina ya ujasiriamali imeanza siku ya Jumatatu ambapo mpaka sasa mada tisa zimekwisha wasilishwa  na inatarajia kufikia kikomo hapo kesho.

Wednesday, 20 April 2016

Semina inogile katika ukumbi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha

Mtaaluma mkuu wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha {AJTC} Bwana Adson Kagiye akiwasilisha mada inayosema Cash Flow Quadrant katika semina ya ujasiriamali inayoendelea chuoni hapo.
Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji  Arusha {AJTC} wameaswa kuweka akiba ili waweze kutumia fursa pindi zinapojitokeza.

Hayo yamesemwa na mtaaluma mkuu wa chuo hicho Bwana Adson Kagiye alipokuwa akiwasilisha mada ya cash flow quadrant katika semina ya ujasiriamali inayoendelea chuoni hapo.

Aidha Bwana Kagiye amewataka wanafunzi kuwa na tabia ya kuweka akiba pamoja na kuwa na malengo huku akiwashauri kutokubali kutumia zaidi ya asilimia 70 ya kipato chao wanachokuwa wamekipata.

Amesema kuwa ili uweze kufanikiwa katika maisha kila mmoja anapaswa kutenga  muda wa kazi  muda wa kulala pamoja na muda wa  kufanya mambo mengine  ya zida.

Kwa upande wake mtoa mada mwingine Bi Jackline Joel ameeleza jinsi uwezo binafsi unavyoweza kuwa ntaji ikiwamo uwezo wa kiakili, nguvu, kiuchumi, pamoja na uwezo wa ubunifu.



Mkufunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha {AJTC} Bi. Jackline Joel akiwasilisha mada inayosema uwezo wako ni mtaji katika semina ya ujasiriamali inayoendelea chuoni hapo
Semina hii ya ujasiriamali imeanza siku ya jumatatu katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha huku mada mbalimbali zikiwasilishwa na wakufunzi wa chuo hicho na inatarajiwa kumalizika siku ya ijumaa ya wiki hii.

Thursday, 14 April 2016

Kashilillah afafanua fedha za madawati


Katibu wa Bunge Thomas Kashilila.


KATIBU wa Bunge, Dk Thomas Kashilillah amesema uamuzi wa Bunge kupeleka fedha Ikulu hautakuwa na athari zozote za uendeshaji wa shughuli za taasisi hizo, kama inavyopotoshwa kupitia mitandao ya kijamii.
Aidha, ameelezea kusitikishwa na taarifa hizo zilizoanza kusambazwa siku chache baada ya Bunge kukabidhi hundi ya Sh bilioni 6 kwa Rais John Magufuli ambazo zimepatikana baada ya Bunge kubana matumizi yake.
Aliyasema hayo jana alipokuwa anazungumzia uamuzi wa kuzipeleka fedha hizo Ikulu kama hautakuwa na athari kwenye bajeti ya Bunge hususan kwenye malipo ya posho na mishahara ya wabunge.
Tayari katika baadhi ya mitandao ya kijamii zipo taarifa zinazodai kuwa ofisi ya Bunge imefikia uamuzi wa kupeleka mabilioni hayo ya fedha Ikulu wakati baadhi ya wabunge wakiwa hawajalipwa posho zao na Bunge lenyewe likiwa linakabiliwa na ukata.
Akizungumzia taarifa hizo, Dk Kashilillah alisema ni taarifa potofu kwa sababu fedha zilizowasilishwa kwa Rais Magufuli ni zile ambazo hazikutumiwa na Bunge kati ya Julai na Oktoba mwaka jana, baada ya kuvunjwa kupisha uchaguzi mkuu.
“Huwa ninapata shida kuzungumzia mambo ya kuokota okota, tulipokuwa tunamkabidhi Rais hizo fedha tulieleza na kama kuna mtu anataka taarifa anapaswa kuuliza mamlaka husika siyo kusambaza uongo.
Ni kweli kwamba tumejibana sana kuokoa fedha hizo lakini pamoja na kujibana huko hizi fedha ni za Bunge la 10 ambalo halikufanya kazi kati ya Julai hadi Oktoba mwaka jana.
“Jumla ya fedha tulizookoa ni Sh bilioni 20, lakini sehemu nyingine za fedha hizo tulitumia kulipa gharama za wabunge wapya kama unavyojua idadi ya wabunge sasa imeongezeka pamoja na shughuli nyingine za Bunge. Zilizobaki zilikuwa lazima zirudi, ndiyo utaratibu ulivyo,” alisema Dk Kashalillah.

Polisi watatu kortini wakituhumiwa kupokea rushwa


Jengo la Mahakama Kuu.


POLISI watatu wa wilayani Urambo, Mkoa wa Tabora wamefikishwa mahakamani kwa mashitaka ya kuomba na kupokea rushwa. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Tabora, iliwafikisha askari hao jana katika Mahakama ya Wilaya ya Urambo huku mwingine akidaiwa kukimbia.

Askari hao waliofukuzwa kazi kabla ya kufikishwa mahakamani ni John Okinda, Kabila Pius na Patrick Robart. Anayedaiwa kukimbia ni Elisha ambaye polisi inaendelea kumtafuta. Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Urambo, Hassan Momba, Wakili wa Takukuru, Edsoni Mapalala alidai washitakiwa walitenda makosa hayo Machi 7 mwaka huu.

Mapalala alidai siku hiyo katika kijiji cha Mkirigi, Kata ya Ilege, Wilaya ya Kaliua, washitakiwa hao wakiwa waajiriwa wa jeshi la polisi, waliomba rushwa ya Sh milioni tatu kutoka kwa Dotto Gandulanye ili wasimchukulie hatua za kisheria baada ya kumkuta akiwa na bangi.

Wednesday, 13 April 2016

Mabalozi watatu wakabidhi hati za utambulisho kwa Rais




Rais Dk John Magufuli.


RAIS John Magufuli amepokea hati za utambulisho za mabalozi watatu wanaoziwakilisha nchini zao hapa nchini. Balozi wa kwanza kukabidhi hati zake za utambulisho ni Carlos Alfonso Puente wa Brazil aliyesema kuwa nchi yake ipo tayari kuimarisha zaidi uhusiano na Tanzania.

Alitaja maeneo ya uzalishaji wa pamba na miwa kuwa ni miongoni mwa yatakayozingatiwa. Kwa upande wake, Rais Magufuli amemhakikishia Balozi Puente kuwa, Serikali itaendelea kushirikiana na nchi yake.

Pia alitaka uwekezaji na biashara kati ya Tanzania na Brazil uimarishwe zaidi, hasa ikizingatiwa kuwa Tanzania inazo rasilimali na fursa nyingi zinazoweza kutumika kwa faida ya pande zote mbili.
Mwingine aliyekabidhi hati zake za utambulisho ni Balozi Pavel Rezac wa Jamhuri ya Czech.

Magufuli ameialika Czech kuungana na Tanzania katika juhudi zake za kuendeleza kilimo na kuzalisha umeme kwa kutumia gesi, ambayo mpaka sasa Tanzania imefanikiwa kugundua uwepo wa futi za ujazo zaidi ya trilioni 57.

Rais Magufuli alimuomba Balozi Rezac kumpelekea salamu Rais wa nchi hiyo, Milos Zeman, kumhakikishia kuwa Serikali yake ya Awamu ya Tano ipo tayari kuimarisha zaidi ushirikiano kukuza biashara na uwekezaji na kujenga uhusiano imara zaidi.

Balozi mwingine aliyewasilisha hati ya utambulisho ni Mariano Deng Ngor wa Sudani Kusini ambaye aliwasilisha salamu za Salva Kiir. Alisema, nchi hiyo itaendeleza na kuimarisha uhusiano na ushirikiano wake na Tanzania.

Aliongeza kuwa, wanaheshimu mchango mkubwa unaotolewa na Tanzania katika kutatua mgogoro wa kisiasa nchini mwao. Rais Magufuli alisema, ataendeleza na kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa kihistoria kati yake na Sudan Kusini.

Alitoa mwito kwa taifa hilo changa kufanya biashara moja kwa moja na Tanzania na nchi nyingine za Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambazo sasa idadi ya watu wake imefikia milioni 165.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli aliagana na Mahadhi Juma Maalim ambaye hivi karibuni alimteua kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kuwait. Balozi Mahadhi anakwenda kuanzisha Ofisi za Ubalozi nchini Kuwait, ikiwa ni moja ya juhudi za Tanzania kuimarisha na kuongeza ushirikiano na uhusiano wake na nchi hiyo ya Mashariki ya Kati.

Tuesday, 12 April 2016

Rais Magufuli aongoza mamia kumuaga mbunge mstaafu


Rais John Magufuli akiaga mwili aliyewahi kuwa Mbunge wa Viti Maalum wa Chadema, Christina Lissu Mughwai katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam jana. ( Picha na Ikulu).

RAIS John Magufuli ameungana na mamia ya waombolezaji kuaga mwili wa Mbunge mstaafu wa Mkoa wa Singida, Marehemu Christina Lissu Mughwai katika ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es Salaam.
Mughwai aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida katika kipindi cha kuanzia mwaka 2010 hadi 2015, aliagwa jana kabla ya kusafirishwa kwenda kijiji cha Mahambe mkoani Singida kwa maziko.
Pamoja na Rais Magufuli na mkewe Mama Janeth, viongozi wengine waliohudhuria shughuli ya kuaga ni Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Akson na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bunge, Freeman Mbowe.
Akitoa salamu kwa niaba ya Rais Magufuli, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene aliwapa pole familia ya marehemu. Alisema katika kipindi chake cha ubunge, Mughwai alitoa mchango mkubwa kama mbunge na kama mtaalamu wa Uchumi.

Sunday, 3 April 2016

Kimeta chaua mmoja, 197 wachunguzwa


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadik.
 
MTU mmoja amefariki kwa ugonjwa wa kimeta wilayani Rombo, huku wengine 197 wakiwa katika uangalizi maalumu na wanne wakitambulika kuugua baada ya kula nyama yenye vimelea vya ugonjwa huo.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadiki amesema ugonjwa huo umeripotiwa katika vijiji vya Ubetu, Wama na Kilongo na wagonjwa wanaendelea na matibabu katika Hospitali Teule ya Huruma.

Sadiki ambaye alifanya ziara katika wilaya hiyo, aliagiza wananchi kutokula nyama za wanyama kama ng’ombe, mbuzi, kondoo na nguruwe bila kuthibitishwa na wataalamu wa afya ili kuepusha kuenea zaidi kwa ugonjwa huo.


Taarifa ya Sadiki iliyotumwa jana na Ofisa Habari wa Mkoa wa Kilimanjaro, Shaban Pazi, ilieleza kuwa kuna uwezekano wa kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro na tayari chanjo kwa mifugo inaendelea.

Alitaka wataalamu wa sekta ya afya kudhibiti uhamishwaji wa mifugo kutoka sehemu moja kwenda nyingine, hususan maeneo ya mipakani na nchi ya Kenya ili kuhakikisha mifugo ya nchini inayopata chanjo haipati maambukizi mengine ya ugonjwa huo.

Umeme warudishia watu zaidi ya bil. 69/-


Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Felix Ngamlagosi
 
 
KUSHUKA kwa bei ya umeme kwa wateja wa kada mbalimbali wa nishati hiyo na kuondolewa kwa tozo ya huduma ya kila mwezi ya Sh 5,520 kwa kila mteja wa nyumbani, kumerudisha kwa Watanzania zaidi ya Sh bilioni 69, iliyokuwa ikienda katika Shirika la Umeme (Tanesco).

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), Felix Ngamlagosi, amesema hayo mwishoni mwa wiki, alipokutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC).

Kwa mujibu wa Ngamlagosi, kufutwa tu kwa tozo ya kila mwezi ya huduma kwa wateja wa majumbani ambayo ilikuwa Sh 5,520, ambayo ni mbali na punguzo la bei kwa kada mbalimbali za wateja, kumewarejeshea Watanzania Sh bilioni 69, ambazo hapo awali zilikuwa zikienda Tanesco.
Alipoulizwa iwapo hatua hiyo ya kupunguza bei ya umeme imetokana na shinikizo kutoka serikalini na kama kutayumbisha shirika hilo muhimu kwa uchumi wa nchi. Ngamlagosi alisema, kwanza maombi ya kushusha bei hiyo yametoka Tanesco.

“Sisi tumepokea barua kutoka Tanesco ikituomba suala la kushusha bei ya umeme na sio kwamba walilazimishwa na Serikali na sisi tuliwahoji sana, kama wataweza kujiendesha, baada ya kuridhika na maelezo yao na uchunguzi wetu, ndipo tukakubali,” alisema Ngamlagosi.

Faida ya gesi Akifafanua matokeo ya uchunguzi uliochangia wakubali kushushwa kwa bei hiyo, Ngamlagosi alisema walibaini ukweli kwamba hivi sasa mitambo ya kuzalisha umeme huo unaouzwa na Tanesco, mingi haitumii tena mafuta, bali inatumia gesi asilia inayochimbwa hapa nchini
Umeme wa mafuta ulikuwa ghali kwa kuwa kwanza yananunuliwa kwa fedha za kigeni na hivyo kuporomoka kwa Shilingi, kuliongeza gharama za ununuzi na pia bei yake kimataifa, ina tabia ya kubadilikabadilika, tofauti na gesi inayochimbwa nchini.

Capacity Charge Ngamlagosi alisema mbali na faida ya kutumia umeme unaotokana na gesi, ambao kwa mujibu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), karibu asilimia 70 ya umeme wote kwa sasa ni wa gesi, pia walibaini mitambo yote ya kufua umeme wa dharura imeondolewa.

“Ni kweli Tanesco hivi sasa wanatumia kiasi kidogo cha mafuta na mitambo yote ya dharura haitumiki tena, pia vyanzo vya nishati vimeongezeka na vingi ni vya uhakika na hakuna kampuni ya dharura ya muda mfupi inayolipwa tozo ya uwezo wa mtambo (capacity charge),” alisema Ngamlagosi.

Tozo hiyo ya uwezo wa mtambo, ambayo ilikuwa ikitozwa katika mitambo mingi ya ufuaji umeme wa dharura, iliongeza gharama kwa kuwa hata kama mtambo hauzalishi au umezimwa kabisa, tozo hiyo ilikuwa ikilipwa kwa siku kwa mabilioni ya Shilingi.

Kutokana na faida hizo, ikiwemo kujaa kwa mabwawa ya kufua umeme wa maji, Ngamlagosi alisema punguzo hilo si hasara kwa sababu unafuu wa uzalishaji nishati hiyo nao umeongezeka.

Wafanyabiashara Wakizungumza na gazeti hili jana, wananchi wa kada mbalimbali nchini wakiwemo wasomi na wanasiasa, wamepongeza Serikali kwa kushusha bei ya umeme na kueleza ni mwanzo mzuri wa wananchi kuanza kufaidi kukua kwa uchumi, huku wakitaka wenye viwanda na wafanyabiashara waangalie namna ya kushusha bei za bidhaa na huduma.

Walisema kwa muda mrefu wananchi wamekuwa wakipata maumivu kutokana na umeme kuwa ghali, jambo lililofanya wengi kutomudu gharama zake wakiwemo wa mijini na vijijini.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana alipongeza Tanesco, Ewura na Serikali kwa punguzo hilo kwani Watanzania wanaanza kufaidi uzalishaji wa umeme kwa gesi asilia inayopatikana nchini na siyo mafuta yaliyokuwa ya gharama kubwa.

Alisema nia ni kumpunguzia mlaji gharama za maisha, kama ilivyo lengo la Serikali ya Awamu ya Tano kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo kwa gharama nafuu. “Kutokana na kupungua gharama hii ya umeme hakika na wazalishaji viwandani watakuwa wamepunguziwa gharama, hivyo ni wakati wa kufikiria kupunguza gharama za bidhaa zao ili kuendelea kumpatia mwananchi wa kawaida unafuu wa maisha,”alisisitiza.

Dk Banna alisema ni dhahiri kuwa uchumi wa nchi ulikuwa ukikua katika vitabu tu huku wananchi wakishindwa kuona manufaa yake lakini sasa wananchi wameanza kufaidi ukuaji wa uchumi wa nchi kwa kuwa na umeme wa uhakika na nafuu. Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba alisema suala la kupungua bei ya umeme ni zuri na linadhihirisha kuwa nchi imepata Rais anayejali wananchi wake.