Mkufunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Bw. Massawe maarufu kwa jina la Kompyuta wizadi akifundisha njia mbalimbali za kutunza kumbukumbu za mapato ya biashara
Bw Massawe ameelezea njia tofauti tofauti ikiwa ni pamoja na kuwa na kitabu mbalimbali vya mapato ambavyo humsaidia mjasiriamali katika kufanya mahesabu ya biashara yake
Wanafunzi wakifanya biashara katika ukumbi wa chuo hicho baada ya kupata semina ya ujasiriamali
Makamo mkuu wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Ausha akifunga semina hii ya ujasiriamali iliyoanza tangu siku ya Jumatatu na kufikia kikomo siku ya leo
Kwa niaba ya mkurugenzi wa mafunzo katika chuo hicho Bw Elifuraha Samboto ambaye ni makamo mkuu wa chuo ametangaza rasmi kufungwa kwa semina hiyo
Amewahasa wanafunzi kutokujiwekea dhana ya kutokuajiriwa pindi wamalizapo chuo kwani baadhi yao baada ya kupata semina hiyo wamekata tamaa ya kutokuajiriwa na kujiajiri wenywe
"Wengi wao wamesema hawataajiriwa na mtu yeyote pindi wamalizapo chuo, hilo wazo ni zuri ila lazima uwe na mtaji wa kujiajiri ,nawshauri wanafunzi waajiriwe ili waweze pata mtaji pia kupata uzoefu wa mambo mbalimbali ya kibiashara"Alisema Bw. Samboto
No comments:
Post a Comment