Semina ya
ujasiriamali imeendelea katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji
Arusha huku mada mbalimbali
zikiwasilishwa na wakufunzi wa chuo hicho.
Muwasilisha mada wa kwanza Bwana Thomas Majaliwa Ishengoma amesema biashara
nyingi zinashindwa kudumu kutokana na ukosefu wa elimu muhimu katika biashara
sanjari na kufanya biashara moja huku akiwashauri wajasiriamali na wanaohitaji
kuwa wajasiriamali kuwa na mazoea ya kujaribu biashara zote.
Mkufunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Bwana Thomas Majaliwa Ishengoma akiwasilisha mada isemayo Ujasiriamali katika semina ya ujasiriamali inayoendelea chuoni hapo. |
Aidha
amesema ili biashara idumu mjasiriamali anapaswa kufanya mambo ambayo yatainua
biashara yake ikiwa ni pamoja na kutengeneza bidhaa yenye thamani kwa wateja
sanjari na kuwa na nguvu ya kifedha.
Kwa upande
wake mtoa mada wa pili Bwana Elifuraha Samboto ameelezea mambo muhimu ya mkakati
wa kimasoko kuwa ni katika kuwalipa na kuwajali wafanyakazi, na kufanya utafiti
wa kibiashara na kuwajali wateja.
Hata hivyo
amesema kuwa mjasiriamali ili aweze kuendelea na kufikia malengo yake anapaswa kuepukana na uvivu, wivu, Chuki,
pamoja na hasira .
Naye mtoa
mada wa tatu Bwana Elihuruma Chao ameelezea kanuni muhimu za mjasiriamali kuwa
ni lazima aipende kazi anayofanya, uwezo wa kusimamia kazi, kuthubutu kufanya
kile ambacho amekusudia pamoja na kuwa na nidhamu katika biashara anayoifanya.
Makamu mkuu wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Bwana Elihuruma chao akiwasilisha mada ya isemayo maadili ya biashara katika semina ya ujasiriamali inayoendelea chuoni hapo. |
Aidha
amesema ili mjasiriamali aendelee mbele lazima afuate maadili ya biashara ambayo
ni kuheshimu hadhi ya kila mfanyakazi, kuwa mwaminifu katika kutoa ahadi za kweli
kwa wateja wake na kuendeleza mahusiano mazuri
kwa wateja wake.
Wanafunzi
wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha wakisikiliza pamoja na
kuandi kakile kinachowasilishwa na wakufunzi wa chuo hicho katika semina
ujasiriamali inayoendelea chuoni hapo.
|
No comments:
Post a Comment