Mtaaluma mkuu wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha {AJTC} Bwana Adson Kagiye akiwasilisha mada inayosema Cash Flow Quadrant katika semina ya ujasiriamali inayoendelea chuoni hapo. |
Wanafunzi wa
chuo cha uandishi wa habari na utangazaji
Arusha {AJTC} wameaswa kuweka akiba ili waweze kutumia fursa pindi
zinapojitokeza.
Hayo
yamesemwa na mtaaluma mkuu wa chuo hicho Bwana Adson Kagiye alipokuwa
akiwasilisha mada ya cash flow quadrant katika semina ya ujasiriamali
inayoendelea chuoni hapo.
Aidha Bwana
Kagiye amewataka wanafunzi kuwa na tabia ya kuweka akiba pamoja na kuwa na
malengo huku akiwashauri kutokubali kutumia zaidi ya asilimia 70 ya kipato chao
wanachokuwa wamekipata.
Amesema kuwa
ili uweze kufanikiwa katika maisha kila mmoja anapaswa kutenga muda wa kazi
muda wa kulala pamoja na muda wa kufanya mambo mengine ya zida.
Kwa upande
wake mtoa mada mwingine Bi Jackline Joel ameeleza jinsi uwezo binafsi
unavyoweza kuwa ntaji ikiwamo uwezo wa kiakili, nguvu, kiuchumi, pamoja na
uwezo wa ubunifu.
Mkufunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha {AJTC} Bi. Jackline Joel akiwasilisha mada inayosema uwezo wako ni mtaji katika semina ya ujasiriamali inayoendelea chuoni hapo |
Semina hii
ya ujasiriamali imeanza siku ya jumatatu katika chuo cha uandishi wa habari na
utangazaji Arusha huku mada mbalimbali zikiwasilishwa na wakufunzi wa chuo
hicho na inatarajiwa kumalizika siku ya ijumaa ya wiki hii.
No comments:
Post a Comment