Darasa la Mbuga ya Ngorongoro katika chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha(Ajtc) wakishangilia mara baada ya kuibuka washindi katika michano ya utangazaji iliyofanyika chuoni hapo. |
Michuano ya utangazaji katika chuo cha uandishi wa habari na utangaza Arusha
(A.J.T.C) imemalizika hii leo ambapo mshindi wa kwanza hadi wa mwisho amejulikana.
Darasa lililoibuka kidedea katika mashindano hayo yaliyochukua takribani siku tano linatambulika kwa jina la Mbuga ya Ngorongorongoro.
Mashindano
hayo aliyohusisha madasa 13, darasa la Ngorongoro limejishindia kombe
lenye thamani ya Tsh 10,000 pamoja na pesa taslimu Tsh 150,000.
Nafasi
ya pili katika michuano hiyo Utangazaji ilichukuliwa na darasa
linaloitwa Mlima Kilimanjaro huku wakijinyakulia tsh10,000 na darasa la
Serengeti limeshikili nafsi ya tatu na kupewa zawdi fedha taslimu Tsh
75,000.
Mkurugenzi wa chuo hicho cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha bw
Joseph Mayagila amewapongeza wanafunzi wote walioshiriki na kuwataka
waendelee kujituma katika masomo yao ili wafanye vizuri katika tasnia ya
uandishi wa habari na utangazaji.
No comments:
Post a Comment