Mashindano ya Utangazaji katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha katika mwaka huu wa 2016 yameenza rasmi siku ya leo.Mashindano haya ni ya 9 tangu kuanzishwa kwa chuo hichi cha utangazaji.Takribani madarasa 13 yatashiriki na leo yameanza madarasa 3.Madarasa hayo ni pamoja na darasa la Selous,Mt. Evarest na darasa la Mt. Meru na mashindano haya ni maalumu kwa wanafunzi wanaosoma katika chuo hicho na lengo kuu la mashindano hayo ni kujifunza na kuwanoa wanafunzi hao ili wanapomaliza chuo wawe na uzoefu wa utangazaji
Mashindano hayo yanatarajia kufikia tamati siku ya Ijumaa ambapo mshindi wa kwanza atajinyakulia Kombe lenye thamani ya sh. 100,000/= na pesa taslimu sh. 150,000/= ,Mshindi wa pili atapata zawadi ya pesa sh. 100,000/= na mshindi wa tatu atapata pesa Sh. 75,000/=
Kesho mashindano yataendelea kwa madarasa yafuatayo;
Darasa la Mt. Udzungwa, kisha darasa la Serengeti na kumaliziwa na darasa la Aicc
Makamo mkuu wa chua cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Bw. Elifuraha Samboto akifungua rasmi mashindano ya utangazaji katika chuo hicho ambaye pia ni Jaji Mkuu katika mashindano hayo
Bw. Elifuraha Samboto akitoa maneno mafupi kabla ya ufunguzi wa mashindano ya utangazaji
Mkuu wa kitengo cha utangazaji katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Bw. Onesmo Mbise akitoa maelekezo kwa wanafunzi jinsi ya kutumia vifaa vya utangazaji kabla ya mashindano kuanza
Mwanafunzi wa darasa la Mt. Meru Theobad Jacob akijaribu vifaa vya utangazaji kabla ya mashindano kuanza
No comments:
Post a Comment