Showing posts with label Habari katika picha. Show all posts
Showing posts with label Habari katika picha. Show all posts

Monday, 23 May 2016

Nani mtani Jembe katika mashindano ya utangazaji ndani ya chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha

Mashindano ya Utangazaji katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha katika mwaka huu wa 2016 yameenza rasmi siku ya leo.Mashindano haya ni ya 9 tangu kuanzishwa kwa chuo hichi cha utangazaji.Takribani madarasa 13 yatashiriki na leo yameanza madarasa 3.Madarasa hayo ni pamoja na darasa la Selous,Mt. Evarest na darasa la Mt. Meru na mashindano haya ni maalumu kwa wanafunzi wanaosoma katika chuo hicho na lengo kuu la mashindano hayo ni kujifunza na  kuwanoa wanafunzi hao ili wanapomaliza chuo wawe na uzoefu wa utangazaji

Mashindano hayo yanatarajia kufikia tamati siku ya Ijumaa ambapo mshindi wa kwanza atajinyakulia Kombe lenye thamani ya sh. 100,000/= na pesa taslimu sh. 150,000/= ,Mshindi wa pili atapata zawadi ya pesa sh. 100,000/= na mshindi wa tatu atapata pesa Sh. 75,000/=


Kesho mashindano yataendelea kwa madarasa yafuatayo;
Darasa la Mt. Udzungwa, kisha darasa la Serengeti na kumaliziwa na darasa la Aicc



















Makamo mkuu wa chua cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Bw. Elifuraha Samboto akifungua rasmi mashindano ya utangazaji katika chuo hicho ambaye pia ni Jaji Mkuu katika mashindano hayo



















Bw. Elifuraha Samboto akitoa maneno mafupi kabla ya ufunguzi wa mashindano ya utangazaji



















Mkuu wa kitengo cha utangazaji katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Bw. Onesmo Mbise akitoa maelekezo kwa wanafunzi jinsi ya kutumia vifaa vya utangazaji kabla ya mashindano kuanza






















Mwanafunzi wa darasa la Mt. Meru Theobad Jacob akijaribu vifaa vya utangazaji kabla ya mashindano kuanza

Tuesday, 19 April 2016

Semina yaendelea kubamba ndani ya chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha (AJTC)

Wanafunzi wa chuo cha uadishi wa habari na utangazaji Arusha [AJTC] wakifuatili kwa umakini mafunzo ya ujasiriamali yanayoendelea chuoni hapo.
Mtaaluma  wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Bwana Adson Mayagila akitoa mafunzo ya ujasiriamali yanayoendelea chuoni hapo.

Mkufunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Bi. Jackline Joel akiwasilisha mada ya ujasiriamali inayoendelea chuoni hapo.

Monday, 18 April 2016

Semina ya ujasiriamali yaaanza katika chuo cha uandishi wa habari Arusha


Mkurugenzi wa mfunzo katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha [AJTC] Bwana Joseph Mayagila akimkaribisha mgeni rasmi Bwana Samwel Senyege katika semina hiyo  iliyoanza hii leo katika ukumbi wa chuo hicho.

Mgeni rasmi  bwana Samwel Senyenye akitoa utangulizi mfupi katika semina ya ujasiriamali iliyofanyika katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha {AJTC} hii leo.

Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha [AJTC] wakifuatilia kwa umakini mafunzo ya ujasiriamali yanayoendelea hii leo katika ukumbi wa chuo hicho

Friday, 11 March 2016

Hatimaye King na Queen wa melody katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha wa mwaka 2016 wamepatikana


















Washindi wa leo katika mashindano ya kumtafuta King & Queen of melody in AJTC 2016 yaliyofanyika katika ukumbi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha



























Malkia wa melody katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha katika mwaka 2016 katika ubora wake jukwaani























Malkia wa melody AJTC 2016




















Mfalme wa melody katika chuo cha uandishi wa habari Arusha 2016 Denis maarufu kwa jina la Mnyalu akihamaki kutangazwa kuwa ni mshindi






















Meza kuu ya majaji katika mashindano hayo




















Picha ya pamoja ya Washindi,Majaji na Waandaaji wa mashindano hayo

Thursday, 10 March 2016

Waandishi wa habari watarajiwa wa upigaji picha

















Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari Arusha (AJTC) wakipata maelekezo jinsi ya Kupiga  picha  za mjongeo (Video) na wa kwanza (kushoto) ni Mwl wa somo hilo Bw. Stephen Mulaki





 















 Mwanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha (AJTC) Alphonce Kusaga akijaribu kuweka camera sawa kabla ya kuanza kazi


 
 















Wanafunzi wakinolewa kwa ajili ya kuja kuwa wapiga picha wazuri wa picha mnato (still picture) na picha mjongeo (video picture)