PHIRI |
Uwezo
unaoonyeshwa na wachezaji wawili wa Yanga, raia wa Zimbabwe, straika
Donald Ngoma na kiungo Thaban Kamusoko, umemfanya kocha wa Mbeya City,
Kinnah Phiri, atangaze kuwa ataongeza straika mmoja kutoka kwenye nchi
hiyo.
Akifafanua
kwa ukina wake, kocha huyo wa zamani wa Free States ya Afrika Kusini,
alisema Zimbabwe ni miongoni mwa nchi zenye wachezaji wengi wenye
viwango vya juu kwenye soka la Tanzania, akiwatolea mfano Ngoma na
Kamusoko walivyotegemeo la Yanga kwa kila kitu.
“Nawajua
vizuri Wazimbabwe, ni moja ya nchi zenye wachezaji wazuri, mfano mzuri
angalia Ngoma na yule mwenzake wanavyofanya vizuri pale Yanga. Pia timu
kama Chicken Inn kuna wachezaji wengi wazuri ambao wanaweza kukusaidia.
“Kikubwa
lazima tuboreshe safu ya ushambuliaji na ningeomba sana kama ningepata
wa kimataifa lakini iwapo viongozi watakataa, hakutakuwa na jinsi
nitasajili humuhumu ingawa kipaumbele zaidi ingekuwa kimataifa,”
alisema.
Katika mikakati yake, amepanga kupata mmoja wa kimataifa na wengine wawili wa kitaifa katika nafasi nyingine.
No comments:
Post a Comment