Thursday, 10 March 2016

Azam yapaa Sauzi, yaahidi ushindi


Wachezaji wa Azam FC wakifanya mazoezi.


TIMU ya soka ya Azam FC ambao ni wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, iliondoka jana kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo wake kwanza dhidi ya Bidvest Wits ya huko.

Tofauti na ilivyozoeleka kwa timu nyingi nchini, Azam jana waliondoka wakiwa na mwonekano tofauti, kwani kuanzia wachezaji hadi viongozi, wamevalia suti zenye nembo ya timu hiyo huku wakibeba mabegi yanayofanana na hivyo kuwafanya waonekane kuwa nadhifu zaidi.

Akizungumza kabla ya kuondoka, nahodha wa timu hiyo John Bocco alisema wanaamini watarejea nyumbani na ushindi. Alisema wachezaji wote walikuwa katika hali nzuri zaidi ya kimchezo na kuwa wameahidi kufanya vema zaidi. Mchezo huo utachezwa keshokutwa.

Aliongeza kuwa, kocha Mwingereza Stewart Hall amewapa mbinu za kisasa za ushindi. “Ushindi ni lazima katika mchezo dhidi ya Bidvest kwani wachezaji na wale wote wanaohusika na hii mechi nguvu tumejipanga kushinda,” alisema Bocco.

Huku Azam ikionekana kujiamini zaidi katika mchezo huo wa keshokutwa, timu ya Bidvest Wits imefikia hatua hiyo ikiwa ni baada ya kuitoa Light Stars ya Shelisheli kwa mabao 9-0. Ilianza kwa kuifunga 3-0 ugenini na kuja kuimalizia kwa 6-0 nyumbani, lakini hata hivyo ukali huo unaonekana kutoiogopesha Azam Fc ambayo imesisitiza inaweza kushinda ugenini.

No comments:

Post a Comment