Aidha, amemuagiza Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Beno Ndulu kupitia upya orodha ya wafanyakazi wa benki hiyo na kuwaondoa mara moja wale wote am bao hawana ulazima wa kuwapo.
Vilevile ameagiza Kitengo cha Madeni ya Nje ambacho awali kilikuwa chini ya Benki Kuu na baadaye kikahamishiwa Wizara ya Fedha, kirejeshwe BoT mara moja kuimarisha udhibiti wa ukopaji na ulipaji wa madeni.
Rais alitoa maagizo hayo jana wakati akizungumza na watendaji wakuu wa Benki wakiwemo, Gavana, Naibu Magavana, Wakurugenzi na Mameneja. Kuhusu ulipaji wa malimbikizo ya malipo, wakati Rais Magufuli akisitisha, tayari BoT ilikuwa katika mchakato wa kufanya malipo ya Sh bilioni 925.6, ambazo Wizara ya Fedha ilitoa idhini yafanyike.
Magufuli ameitaka Wizara ya Fedha ifanye upya uhakiki wa malipo hayo, kubaini kama walengwa walioidhinishwa kulipwa wanastahili kuyapata au la. Kwa upande wa wafanyakazi, Rais Magufuli amemuagiza Gavana wa BoT, Profesa Beno Ndulu kupitia upya orodha ya wafanyakazi wa benki hiyo na kuwaondoa mara moja wote ambao hawana ulazima wa kuwa wafanyakazi katika benki hiyo.
“Haiwezekani tukawa na kundi kubwa la wafanyakazi, wanalipwa mishahara wakati hata kazi wanazofanya hazijulikani,” alisema Magufuli. BoT imetajwa kuwa ina wafanyakazi 1,391.
Wakati Rais Magufuli akitoa agizo hilo la kutaka orodha ya wafanyakazi ipitiwe upya, Benki hiyo imekuwa ikituhumiwa kuajiri watoto wengi wa vigogo, jambo ambalo liliwahi kuibua mjadala kwenye mitandao ya kijamii, huku baadhi ya majina ya vigogo hao yakiwekwa hadharani.
Wakati huo huo, Rais ameagiza Kitengo cha Madeni ya Nje ambacho awali kilikuwa chini ya Benki Kuu na baadaye kikahamishiwa Wizara ya Fedha, kirejeshwe BoT mara moja kuimarisha udhibiti wa ukopaji na ulipaji wa madeni.
No comments:
Post a Comment