Wednesday, 9 March 2016

Wafanyabiashara wa soko la kwa Morombo wagoma kuhama



 














Mwenekiti wa mtaa wa FFU Bw Anaclet Edward
 



















 Bi. Regina Makorongo akichochea moto


 
















Mfanyabiashara wa soko la kwa morombo jijini Arusha Zena Shabaan


 Wafanyabiashara wa soko la kwa Morombo wamegomea manispaa ya jiji la Arusha kuhamimia katika eneo lililotengwa na serikali na kusema hawako tayari kutokana na miundo mbinu ya soko hilo kuwa mibovu na  kuhofia usalama wa mali zao
Hata hivyo amesema kuwa mtu anapokamatwa na manispaa anatakiwa apelekwe mahakamani na siyo mahali pengine  na kuiomba serikali  hii ya awamu ya tano iwatengenezee mazingira mazuri ya biashara
“Yaani hawa manispaa wanatunyanyasa kwa kweli, sisi kufanya biashara zetu pembezoni mwa barabara ni kutokana na mazingira ya soko ambalo walitupeleka kuwa mibovu na hakuna ulinzi wowote ambao utaweka hali ya usalama tunalipa kodi sasa hizo pesa zetu za kodi wanazipeleka wapi ?” Alisema mmoja wa wafanyabiashara
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa  wa FFU  ambako linapatikanaa soko hilo Bw. Anaclet Edward amesema  kuwa eneo wanalofanyia biashara kwa sasa ni kinyume cha sheria  kwani mwaka jana walipewa barua ya maandishi wahame eneo hilo lakini cha kushangaza hadi sasa wapo wanaendelea na biashara
Sanjari na hayo Bw. Edward ameongeza kwa kusema yeye hawanyanyasi wananchi  wake bali anatekeleza jukumu hilo kwa manufaa yao wenyewe
“Mimi nafanya hivyo kwa ajili ya kuwaweka kwenye usalama kwa siyo tu ni amri kutoka manispaa ya jiji letu hili cha msingi wananchi wafuate kanuni  na utaratibu unavyotaka”Aliongea mwenyekiti huo

No comments:

Post a Comment