Fedha hizo zimetolewa licha ya Stars kufungwa 2-1 na Zimbabwe mwishoni mwa wiki iliyopita, jijini Dar es Salaam. Awali, wachezaji wa timu hiyo waliahidiwa kupewa kiasi kama hicho kama wangeishinda Zimbabwe katika kila mchezo, wa nyumbani na ugenini.
Lakini jana, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura aliyechangisha kiasi cha Sh milioni 17 kutoka kwa wadau mbalimbali, aliamua kutoa Sh 300,000 kwa wachezaji 25 ili kuwaongezea motisha ya kushinda ugenini. Endapo watashinda wiki ijayo, watakabidhiwa pia kitita kama hicho kwa kila mchezaji.
Akizungumza na wachezaji hao Dar es Salaam jana, Naibu waziri huyo alisema; “Najua ahadi ilikuwa mkishinda ndio tugawane hizi fedha, lakini nime- Namua niwape na naamini itazidisha hamasa katika mechi ya marudiano naamini mtashinda na kumalizia kugawana kiasi kilichobaki.
“Lakini pia leo tunaadhimisha siku ya wanawake duniani, hivyo si vibaya nanyi mkaungana na wanawake wengine katika kusherehekea siku hiyo kwa motisha hii kidogo,” alisema. Twiga Stars inatarajia kuondoka nchini Machi 17 kwenda Zimbabwe kwa ajili ya mechi ya marudiano. Timu itakayofuzu hatua inayofuata itacheza na mshindi wa mechi kati ya Zambia na Namibia.
No comments:
Post a Comment