Mkuu wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Bw Joseph Mayagila akijibu swali lililoulizwa na mwanafunzi katika semina ya ujasiriamali iliyofanyika katika ukumbi wa chuo hicho
Mkuu wa chuo cha AJTC Joseph Mayagila akiwa ofisini kwake
Mkuu wa chuo cha uandishi
wa habari na utangazaji Arusha Bw
Joseph Mayagila
Amewataka wajasiriamali kufanya utafiti wa masoko kabla ya
kufungua biashara
Ameyasema hayo katika semina ya ujasiriamali iliyofanyika
katika ukumbi wa chuo hicho wakati alipojibu swali la mwanafunzi wa chuo hicho Bi Anna Elias alipotaka
kujua jinsi ya kufungua biashara na kuweza kuwa mjasiriamali mkubwa duniani
“Ili uweze kutoka kibiashara unatakiwa ujue soko lako pia
lazima ujue wateja wako ni wakina
nani,kuanzia ubora na udhaifu na mengine yanayohusu wateja” Alisema Bw Mayagila
Hata hivyo amesema
ili ufanye biashara unatakiwa ufikirie mambo makubwa yatakayo kusaidia
na uwe na uelewa wa kutosha kuhusu
biashara yako
Ameongeza kwa kusema kuwa mjasiriamali mzuri ni yyule
anayependa kuwafundisha waliochini yake kimadaraka ili anaposhindwa mahali
Fulani waweze kumsaidia
Pia amesema semina za
ujasiriamali zinazotolewa cguoni hapo zimeweza kuwasaidia wanafunzi wengi
kutoka kimaisha pasipo kutegemea kuajiriwa pindi wanapomaliza chuo
No comments:
Post a Comment