Afisa ustawi wa jamii Bw. Shija Numbu |
Wazazi wamehaswa kuwalea watoto wao pindi wanapokuwa wadogo
hadi wanapofikia umri wa miaka 18 na kuwapa huduma za msingi ambazo mtoto
anazihitaji
Hayo yamesemwa na Afisa Ustawi wa Jamii Bw. Shija Numbu
wakati akizungumza na mmiliki wa blog hii na kulezea kwa undani zaidi kuhusu
majukumu ya mzazi kwa mtoto kwa mujibu wa sheria za haki za watoto ya mwaka 2009
Amesema kwamba sheria hii inawataka wazazi kuwapa watoto
elimu,malezi mazuri bila kusahau afya bora na kuhakikisha mtoto anakuwa katika muonekano
mzuri
Mbali na hayo pia amesema kwamba ni kosa la jinai kwa mzazi
kumuozesha mtoto wa kike aliyechini ya umri wa miaka 18 kwani atasababisha
mtoto huyo kukosa haki ya kupata elimu pia kusababisha kupata madhara kwa kubeba mimba za utotoni
“Mtoto akiolewa chini ya umri wa miaka 18 kawaida viungo
vyake vya uzazi vinakuwa bado havijakaza
hivyo akibeba mimba nirahisi sana kupata saratani ya kizazi “Alisema Bw. Shija
Hata hivyo amesema kuwa wazazi ndiyo ngazi ya kwanza katika kupinga ndoa za utotoni pindi
wanapoona watoto wao wanakwenda ndivyo sivyo ili waweze kuwasaidia kutimiza
ndoto zao
Vilevile Bw. Numbu amezungumzia suala zima la ukeketaji kwa
watoto na kusema kuwa dhana hiyo bado inaendelea katika mkoa wa Arusha na kwa sasa wanatumia njia mbadala katika
kutizimiza adha hiyo ya ukeketaji kwa watoto
“Kwa sasa wanawakeketa watoto wakiwa wachanga hivyo mtu si
rahisi kujua kwa sababu wanaogopa
kutumia njia ya zamani kwa kuwa
watajulikana hivyo bado tunaendelea
kutoa elimu kwa jamii ili kuhakikisha tunatokomeza dhana hii katika jamii”
Alisema Numbu
Amesema kuwa hawajawahi kupokea kesi ya ukeketaji kwa
wanawake katika ofisi zao kwa sababu
jamii inogopa kwa kuhofia kuchukuliwa
hatua za kisheria lakini mwaka 2012 walipokea kesi moja ya ndoa za utotoni na hadi sasa hivi hakuna kesi yeyote waliyowahi
kupokea kuhusana na ndoa za utotoni pamoja na ukeketaji
No comments:
Post a Comment