Tuesday, 23 February 2016

Simba yaibuka kidedea katika kombe la nani mtani jembe





 















Timu ya Simba wakijiandaa  wakijiandaa na kupiga penati


 















 Wakiwa katika mapumziko ya Kipindi cha kwanza

















 Kikosi na mashabiki wa timu ya Simba wakiondoka uwanjani kwa mbwembwe  baada ya kuikung`uta Yanga goli 7 kwa nunge




Mashindano ya nani mtani jembe kati ya mashabiki wa  timu ya Yanga na Simba  katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha yametia nanga kwa timu ya simba kushinda mabao 7-0 mechi iliyochezwa katika viunga vya uwanja wa field fource kwa Morombo

Ambapo  magoli hayo ya Simba yaliwekwa kimiani  na mshambuliaji machachari Calvin Stanley ambaye alifunga magoli 3 huku magoli 2 yaliwekwa wavuni na kiungo mkabaji Jackson Mabula na goli moja kufungwa na golikipa Benson

Kwa upande wake kocha wa timu ya Yanga Proti Mmanga amesema timu yake ilizidiwa kutokana na wachezaji wake kupungua uwanjani baada ya  mchezaji wake Kephas Ilan kupewa kadi nyekundu kutoana na kuchezea rafu golikipa wa Simba Benson

Na mchezoo huo ulikuwa ukiongozwa na Refa Geog Silange hadi mwisho wa mchezo








No comments:

Post a Comment