Monday, 22 February 2016

WANAFUNZI KATIKA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI ARUSHA(AJTC)WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI ZAIDI KATIKA MASOMO YAO

Jengo la utawala katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji arusha.

Wanafunzi katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji arusha(AJTC)wametakiwa kuongengeza juhudi katika masomo yao ili waweze kufanya vizuri kwa ajili ya  kukabiliana na soko la ajira hapa nchini.

Akizungumza na mwandishi wetu  mtaaluma katika chuo hicho bi.jackline amesema kuwa wanafunzi wote wanatakiwa kujituma katika kujisomea na kufanya mazoezi ya vitendo kila siku kwa ajili ya kukabiliana na soko la ajira hapa nchini.

Mtaaluma katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji arusha (AJTC) Bi.jackline akiendelea na majukumu yake ya kila siku ofisini kwake.


Aliongeza na kusema kuwa wanafunzi wakifanya mazoezi ya vitendo hii itawasaidia kujiimarisha zaidi katika tasnia hii ya habari na watafanya vizuri zaidi pale watakapokwenda kufanya kazi katika vyombo mbalimbali vya habari.

Hata hivyo aliwataka wanafunzi ambao wanajikita katika baadhi ya masomo na kubagua masomo mengine waache mara moja kwani fani ya uandishi wa habari na utangazaji inajumuisha masoma mbalimbali ambayo yatawasaidia katika jamii.
 

wanafunzi wakiwa darasani wakiendelea na mafunzo ya vitendo,kushoto ni emmanuery minja akiwa na happy kalemerwa


kwa upande wake emmanuery minja ambaye ni mwanafunzi wa astashahada  chuoni hapo amesema kuwa wanafunzi wengi wamekua wakijisahau kupitia vitabu mbalimbali lakini pindi mitihani inapokaribia ndipo wanajikita zaidi katika kujisomea.

vilevile ameongeza na kuwaomba wanafunzi wenzake wajitahidi kufanya mazoezi ya vitendo kwa kusoma taarifa za habari,kuandaa vipindi maalumu na hata vipindi mbalimbali  vya burudani hii itawasaidia kufanya vizuri zaidi katika tasnia hii.

No comments:

Post a Comment