Tuesday, 9 February 2016

WAFANYABISHARA JIJINI ARUSHA WAIOMBA SERIKALI IWABORESHEE MAENEO YAO YA KUDUMU YA BIASHARA








 Kushoto ni  Bi.Halima akielezea matatizo wanayokumbana  nayo katika harakati zake za biashara (kulia) ni Bw Samson Festo.





 Bi. Halima akitabasabu na Bw. Samson Festo katika mazungumzo mawili matatu na Bw Samson Festo


Wafanyabiashara  wa soko la kwa Morombo wameiomba serikali iwasaidie kuboresha soko hilo lililopo mtaa wa Murieti ili wawezeepukana na adha za usumbufu kati yao na manispaa ya jiji hilo la Arusha
Akizungumza kwa niaba ya wafanyabiashara wa soko hilo Bi. Halima ameyasema hayo  mapema leo wakati akizungumza na mmiliki wa blog hii na kuelezea hisia wanazopata pindi manispa ya jiji wanapokuja kuwafukuza maeneo wanayofanyia biashara zao kwa sasa.
“Sisi tumekuwa kama wakimbizi kwa kweli kwa sababu tunafukuzwa mahali tunapojipatia kipato sasa sisi twende wapi,hata kama  biashara zetu tunazifanyia pembezoni mwa barabara hawawezi kutufukuza kama mbuzi bwana”
Sanjari  na hayo Bi. Halima amesema kuwa eneo lililotengwa  na serikali kwa  ajili ya biashara lipo lakini haliridhishi hasa katika kipindi hiki cha mvua  maji yanatuma  hivyo kupelekea kukosa wateja  wa biashara zao wanazozifanya sokoni hapo.
Vilevile akaongezeaa kwa kusema  kuwa mbali na kutuama kwa maji kipindi cha mvua amesema kwamba sasa hivi bado kuna ugonjwa  wa kipindupindu hivyo kwenda kufanyia biashara eneo hilo kunaweza kuibua ugonjwa huo kutokana na mazingira hayo kutokuwa rafiki na watumiaji wa soko hilo la wa Morombo.
Kwa upande wake mwenyekiti  wa mtaa huo Bw Anaclet R Edward amesema kwamba  lengo la manispaa kuwazuia kufanyia biashara pembezoni mwa barabara ni kwa masilahi yao binafsi na siyo serikali kwa  sababu eneo hilo ni hatari kwa maisha yao
Pia amesema kuwa  serikali imetenga eneo la soko kwa ajali ya wafanyabiashara hao ila miundo mbinu ya eneo hilo ni tatizo na limekuwa ni changamoto wa upande wake na serikali nzima ya mtaa huo
Hata hivyo amesema suala hilo linashughulikiwa na manispaa ya jiji la Arusha  katika kuhakikisha mazingira ya soko hilo yanakuwa rafiki wa wafanyabiashara na watumiaji wa soko kwa ujumla

No comments:

Post a Comment