Mkufunzi na mkuu wa kitengo cha utangazaji katika chuo cha uandishi wa habariutangazaji Arusha Bw Onesmo Mbise
Mkufunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha
na ambaye pia ni mkuu wa kitengo cha Radio ya chuo hicho kinachojulikana kwa
jina la AJTC Radio Bw. Onesmo Mbise amewataka wanafunzi wajiandae kwa mazoezi
ya vitendo kabla ya kuingia katika bonanza la utangazaji chuoni hapo
Hayo yamejiri wakati akizungumza na wanafunzi katika ukumbi wa chuo hicho na kuwapa maagizo
hayo ambapo bonanza hilo linatarajia kuanza mnamo tar 03/5/2016 katika studio
hizo zilizopo katika eneo la chuo hicho
Bw Mbise amesema madarasa yote yanayopatikana katika chuo
hicho ni lazima yashiriki katika mashindano hayo na kusema zawadi za kipindi
hiki zimeboreshwa siyo kama za mwaka
jana ambapo mshindi wa kwanza alikuwa akipewa Kombe lenye thamani ya 100,000
pamoja shilingi 70,000 na mshindi wa pili akiambulia pesa tasilimu sh 50,000
huku mshindi wa tatu akipewa kreti la soda
“Mwaka huu tumejipanga vizuri na lengo la mashindano haya ni
kuinua vipaji vya wanafunzi wetu ili wanapo maliza chuo wakawe wazuri katika
kuwasilisha vipindi vyao”Aisema Mkufunzi huyo.
Kila mwaka kumekuwa na mashindano hayo ya utangazaji kama tulivyoona mwaka jana mshindi wa kwanza
lilikuwa ni darasa la Ruaha(Diploma) waliondoa na kombe huku mshindi wa pili
likiwa ni darasa la Mr Meru(Diploma) na mshindi wa tatu likiwa ni darasa la
Katavi(Certificate)
No comments:
Post a Comment