Tuesday, 9 February 2016

SIMBA YAITISHA STAND UNITED, YAPIGA MTU 3-0

KUELEKEA mechi dhidi ya Stand United na Simba  itakayochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Kambarage, Simba leo imeifunga Miatu Kombaini ya wilayani Bariadi bao 3-0.


Mechi hiyo ya kirafiki imechezwa wilayani humo ambapo mabao ya Simba yalifungwa na Danny Lyanga, Musa Mgosi na Said Ndemla wachezaji ambao wote huanzia benchi. 

Simba watacheza na Stand United ukiwa ni mchezo wao wa pili Kanda ya Ziwa katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara ambapo mchezo uliopita dhidi ya Kagera Sugar uliochezwa Uwanja wa Kambarage walishinda bao 1-0.

Kocha wa Simba, Jackson Mayanja alisema kuwa ameamua kuwatumia wachezaji ambao hawapati nafasi ya kucheza mara kwa mara ili kuwaweka fiti kwani muda wowote atawatumia kwenye mechi zijazo.

"Naamini nina wachezaji wazuri kwenye kikosi changu na kila mmoja atakayejituma atapata nafasi ya kucheza, Simba hii si ya mtu mmoja," alisema Mayanja

No comments:

Post a Comment