Wednesday, 17 February 2016

WANANCHI WA MANISPAA YA JIJI LA ARUSHA WATAKIWA KULIPIA USHURU WA TAKATAKA

Taka zikiwa zimelundikana katika mtaa wa Olasiti


Vijana wakipakia taka kwenye gari


Msimamizi wa Taka katika mtaa wa Burka na Orekeriani Bi Rahma Lymo



Wananchi  wa manispaa ya Jiji la Arusha wametakiwa kulipia ushuru wa takataka  mapema iwezekanavyo kabla ya kufikia  siku ya Jumanne ya tarehe 23 mwezi wa pili mwaka huu

Kauli hiyo imetolewa na msimamizi wa  taka kaitka mtaa wa Burka na Orekerini Bi Rahma Lymo mapema leo Mchana wakati walipokuja kuchukua takataka maeneo tofautitofauti  inayozunguka Manispaa ya jiji hilo la Arusha 

Bi.  Rahma ambaye anafanya kazi hiyo katika kampuni ya Mazingira Group amesema ifikapo Jumanne ya tar. 23 mwezi huu wa pii mwaka 2016 wataagiza migambo wa manispaa kuwakamata  wale ambao hawajalipia ushuru huo na faini itakuwa ni  50,000Tsh na faini hiyo haitajumuishwa na deni analodaiwa mtu

“Wananchi wamekuwa wagumu kuheshimu kazi za watu hivyo hatuna budi kutuma migambo wa manispaa kuwafuatilia wananchi hao wazembe, utakuta mtu hajalipia miezi mitano sasa unafikiri sisi tutafanyaj  kazi kama hawatulipi pesa kumbuka tunatumia usafiri” Alisema bi Rahma

 Vilevile ameeleza kuwa zimepita wiki Tatu bila ya kuja kuchukua taka mitaa mbalimbali ya manispaa hiyo chanzo kikiwa ni kutokulipwa na wakazi wa maeneo husika hivyo kupelekea mitaa mbalimbali kuonekana michafu ambayo inaweza kupelekea milipuko ya magonjwa yatokanayo na uchafu

Hata hvyo amewaomba wananchi kupenda kulipia ushuru huo bila shuruti ili kukwepa adha mbalimbali kwani  kwa mwezi wanalipia Tsh 2,000 kwa kaya moja















No comments:

Post a Comment