Muonekano wa mapango ya Amboni yanayopatiana mkoani Tanga
Vijana wakiwa wanatoka ndani ya mapango ya Amboni
Mapango ya amboni ni moja ya vivutio vikubwa vya kitalii
nchini kwani yamekuwa yakipokea wageni tofauti tofauti wa ndani na nje ya nchi
Mpango haya yanapatikana katika kijiji cha Kiyomoni kata ya Amboni mkoani Tanga na inasemekana mapango haya
yalikuwepo tangu miaka milioni 100 na 50(100,500,000) iliyopita
Miamba hii ilitokea baada ya tetemeko la ardhi
miaka hiyo na katika mapango hayo kuna miamba ya chokaa ambapo miamba hii inasaidia katika menginea
shughuli za kiwandani kwa ajili ya kutengenezea chokaa ambazo zinatumika katika
ujenzi na mambo
Akizungumzia historia hiyo ya mapango ya Amboni Bw. Allan
amesema kwamba eneo hili lina ukubwa wa kilomita za mraba zipatazo 234
“Pia ndani ya miamba hii kulishawahi kupotea mzungu ambaye
alikataa kuongozwa na mwenyeji wa eneo hili alipoingia mapangoni hajatoka hadi
leo hii tangu miaka 8 iliyopita mzungu huyo aliingia na mbwa wake cha ajabu
mbwa tulimuona na mzungu huyo hakuonekana na inasemekana kwamba aliingia kwenye
mashimo ambayo yanaelekea mlima Kilimanjaro na kupotelea huko”Alisema Allan
No comments:
Post a Comment