Halikadhalika, kamati za shule wilayani Temeke zimeanza kupewa mafunzo ya jinsi ya kutumia fedha zinazotolewa na Halmashauri kwa ajili ya ujenzi huo.
Akitoa taarifa hiyo jana, Ofisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda, alisema makandarasi wa ujenzi, wameshaanza kufanya vipimo katika maeneo ya ujenzi wa vyumba vya nyongeza 10 kwa shule zilizofurika wanafunzi na nyingine kujenga madarasa matano.
Mapunda alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo amekutana jana na kamati za shule wilayani Temeke ili kupata mafunzo, jinsi watakavyotumia fedha katika ujenzi wa vyumba hivyo.
Alisema baada ya mafunzo hayo, shule zitapelekewa fedha ili kuanza ujenzi katika Halmashauri hiyo na kufuatiwa na manispaa za Ilala na Kinondoni.
Awali, Mkuu wa Mkoa, Said Mecky Sadiki alisema mkoa una ongezeko la wanafunzi asilimia 117. Akitoa mfano alisema shule ya Msongola wanaotakiwa ni wanafunzi 200, lakini wameandikisha 720, Kivule wanaotakiwa ni 250 lakini wameandikisha 710.
No comments:
Post a Comment