Friday, 22 April 2016

semina ya ujasiriamali yafika tamati katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha ndani ya mwaka huu wa 2016















Mkufunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Bw. Massawe maarufu kwa jina la Kompyuta wizadi akifundisha njia mbalimbali za kutunza kumbukumbu za mapato ya biashara



Bw Massawe ameelezea njia tofauti tofauti ikiwa ni pamoja na kuwa na kitabu mbalimbali vya mapato ambavyo humsaidia mjasiriamali katika kufanya mahesabu ya biashara yake
























Wanafunzi wakifanya biashara katika ukumbi wa chuo hicho  baada ya kupata semina ya ujasiriamali




Makamo mkuu wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Ausha akifunga semina hii ya ujasiriamali iliyoanza tangu siku ya Jumatatu na kufikia kikomo siku ya leo



Kwa niaba ya mkurugenzi wa mafunzo katika chuo hicho Bw Elifuraha Samboto  ambaye ni makamo mkuu wa chuo ametangaza rasmi kufungwa kwa semina hiyo


Amewahasa wanafunzi kutokujiwekea dhana ya kutokuajiriwa pindi wamalizapo chuo kwani baadhi yao baada ya kupata semina hiyo wamekata tamaa ya kutokuajiriwa na kujiajiri wenywe

"Wengi wao wamesema hawataajiriwa na mtu yeyote pindi wamalizapo chuo, hilo wazo ni zuri ila lazima uwe na mtaji wa kujiajiri ,nawshauri  wanafunzi waajiriwe ili waweze pata mtaji pia kupata uzoefu wa mambo mbalimbali ya kibiashara"Alisema Bw. Samboto





Thursday, 21 April 2016

Je wajua mpango mkakati wa masoko?

Semina ya ujasiriamali imeendelea katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha  huku mada mbalimbali zikiwasilishwa na wakufunzi wa chuo hicho.

Muwasilisha  mada wa kwanza Bwana Thomas Majaliwa Ishengoma amesema biashara nyingi zinashindwa kudumu kutokana na ukosefu wa elimu muhimu katika biashara sanjari na kufanya biashara moja huku akiwashauri wajasiriamali na wanaohitaji kuwa wajasiriamali kuwa na mazoea ya kujaribu biashara zote.

Mkufunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Bwana Thomas Majaliwa Ishengoma akiwasilisha mada isemayo Ujasiriamali  katika semina ya ujasiriamali inayoendelea chuoni hapo.
Aidha amesema ili biashara idumu mjasiriamali anapaswa kufanya mambo ambayo yatainua biashara yake ikiwa ni pamoja na kutengeneza bidhaa yenye thamani kwa wateja sanjari na kuwa na nguvu ya kifedha.

Kwa upande wake mtoa mada wa pili Bwana Elifuraha Samboto ameelezea mambo muhimu ya mkakati wa kimasoko kuwa ni katika kuwalipa na kuwajali wafanyakazi, na kufanya utafiti wa kibiashara na kuwajali wateja.
Mkufunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Bwana Elifuraha Samboto akiwasilisha mada ya isemayo mkakati wa kukuza soko la biashara katika semina ya ujasiriamali inayoendelea chuoni hapo.
Hata hivyo amesema kuwa mjasiriamali ili aweze kuendelea na kufikia malengo yake anapaswa kuepukana na uvivu, wivu, Chuki, pamoja na hasira .

Naye mtoa mada wa tatu Bwana Elihuruma Chao ameelezea kanuni muhimu za mjasiriamali kuwa ni lazima aipende kazi anayofanya, uwezo wa kusimamia kazi, kuthubutu kufanya kile ambacho amekusudia pamoja na kuwa na nidhamu katika biashara anayoifanya.

Makamu mkuu  wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Bwana Elihuruma chao akiwasilisha mada ya isemayo maadili ya biashara katika semina ya ujasiriamali inayoendelea chuoni hapo.
Aidha amesema ili mjasiriamali aendelee mbele lazima afuate maadili ya biashara ambayo ni kuheshimu hadhi ya kila mfanyakazi, kuwa mwaminifu katika kutoa ahadi za kweli kwa wateja wake na kuendeleza mahusiano mazuri  kwa wateja wake.
Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha wakisikiliza pamoja na kuandi kakile kinachowasilishwa  na wakufunzi wa chuo hicho katika semina ujasiriamali inayoendelea chuoni hapo.
Semina ya ujasiriamali imeanza siku ya Jumatatu ambapo mpaka sasa mada tisa zimekwisha wasilishwa  na inatarajia kufikia kikomo hapo kesho.

Wednesday, 20 April 2016

Semina inogile katika ukumbi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha

Mtaaluma mkuu wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha {AJTC} Bwana Adson Kagiye akiwasilisha mada inayosema Cash Flow Quadrant katika semina ya ujasiriamali inayoendelea chuoni hapo.
Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji  Arusha {AJTC} wameaswa kuweka akiba ili waweze kutumia fursa pindi zinapojitokeza.

Hayo yamesemwa na mtaaluma mkuu wa chuo hicho Bwana Adson Kagiye alipokuwa akiwasilisha mada ya cash flow quadrant katika semina ya ujasiriamali inayoendelea chuoni hapo.

Aidha Bwana Kagiye amewataka wanafunzi kuwa na tabia ya kuweka akiba pamoja na kuwa na malengo huku akiwashauri kutokubali kutumia zaidi ya asilimia 70 ya kipato chao wanachokuwa wamekipata.

Amesema kuwa ili uweze kufanikiwa katika maisha kila mmoja anapaswa kutenga  muda wa kazi  muda wa kulala pamoja na muda wa  kufanya mambo mengine  ya zida.

Kwa upande wake mtoa mada mwingine Bi Jackline Joel ameeleza jinsi uwezo binafsi unavyoweza kuwa ntaji ikiwamo uwezo wa kiakili, nguvu, kiuchumi, pamoja na uwezo wa ubunifu.



Mkufunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha {AJTC} Bi. Jackline Joel akiwasilisha mada inayosema uwezo wako ni mtaji katika semina ya ujasiriamali inayoendelea chuoni hapo
Semina hii ya ujasiriamali imeanza siku ya jumatatu katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha huku mada mbalimbali zikiwasilishwa na wakufunzi wa chuo hicho na inatarajiwa kumalizika siku ya ijumaa ya wiki hii.

Tuesday, 19 April 2016

Semina yaendelea kubamba ndani ya chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha (AJTC)

Wanafunzi wa chuo cha uadishi wa habari na utangazaji Arusha [AJTC] wakifuatili kwa umakini mafunzo ya ujasiriamali yanayoendelea chuoni hapo.
Mtaaluma  wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Bwana Adson Mayagila akitoa mafunzo ya ujasiriamali yanayoendelea chuoni hapo.

Mkufunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Bi. Jackline Joel akiwasilisha mada ya ujasiriamali inayoendelea chuoni hapo.

Monday, 18 April 2016

Semina ya ujasiriamali yaaanza katika chuo cha uandishi wa habari Arusha


Mkurugenzi wa mfunzo katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha [AJTC] Bwana Joseph Mayagila akimkaribisha mgeni rasmi Bwana Samwel Senyege katika semina hiyo  iliyoanza hii leo katika ukumbi wa chuo hicho.

Mgeni rasmi  bwana Samwel Senyenye akitoa utangulizi mfupi katika semina ya ujasiriamali iliyofanyika katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha {AJTC} hii leo.

Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha [AJTC] wakifuatilia kwa umakini mafunzo ya ujasiriamali yanayoendelea hii leo katika ukumbi wa chuo hicho

Thursday, 14 April 2016

Yanga, Azam zatakata



Mchezaji wa Yanga Issoufour Boubacar akimtoka mchezaji wa timu ya Mwadui, Jabir Aziz wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam jana. Yanga ilishinda mabao 2-1.


TIMU ya Yanga na Azam zimeng’ara katika Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kushinda katika michezo yao ya viporo iliyofanyika jana.
Yanga iliifunga Mwadui FC ya Shinyanga mabao 2-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Azam FC ilifunga Mtibwa Sugar bao 1-0 Uwanja wa Manungu, Turiani.

Azam imemaliza mechi zake za viporo, ambapo imecheza mechi 24 ikiwa na pointi 55 ikishika nafasi ya tatu nyuma ya Yanga iliyocheza mechi 23 ikiwa na pointi 56.
Yanga itamaliza mechi yake ya viporo Jumamosi dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Simba ndiyo inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 57 baada ya kucheza mechi 24.
Mashabiki wa Yanga ilibidi wasubiri hadi dakika ya 86 kushangilia kwa nguvu bao la pili lililowahakikishia ushindi, mfungaji akiwa Haruna Niyonzima, baada ya kumalizia mpira uliookolewa na mabeki wa Mwadui.

Kabla ya bao hilo, Mwadui ilipata pigo baada ya Iddy Mobby kutolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu Donald Ngoma.

Yanga ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya tatu mfungaji akiwa Simon Msuva akiunganisha kwa kichwa krosi ya Oscar Joshua.

Hata hivyo, bao hilo halikudumu sana kwani dakika ya 13 Mwadui ilisawazisha mfungaji akiwa Kelvin Kabati aliyetumia vyema makosa ya mabeki wa Yanga waliojichanganya.
Timu hizo ziliendelea kushambuliana kwa zamu, lakini umakini wa washambuliaji ulikuwa kikwazo kila walipoingia katika eneo la hatari.

Katika mchezo wa Mtibwa Sugar, washindi walipata bao hilo pekee mfungaji akiwa nahodha wa timu hiyo, John Bocco.

Azam ingeweza kupata mabao zaidi, lakini washambuliaji wake walishikwa na kigugumizi kila walipokaribia lango la wapinzani wao, hali ambayo pia iliikuta Mtibwa Sugar.
Matokeo hayo yameifanya Mtibwa Sugar ibaki nafasi ya nne ikiwa na pointi 34.

Kashilillah afafanua fedha za madawati


Katibu wa Bunge Thomas Kashilila.


KATIBU wa Bunge, Dk Thomas Kashilillah amesema uamuzi wa Bunge kupeleka fedha Ikulu hautakuwa na athari zozote za uendeshaji wa shughuli za taasisi hizo, kama inavyopotoshwa kupitia mitandao ya kijamii.
Aidha, ameelezea kusitikishwa na taarifa hizo zilizoanza kusambazwa siku chache baada ya Bunge kukabidhi hundi ya Sh bilioni 6 kwa Rais John Magufuli ambazo zimepatikana baada ya Bunge kubana matumizi yake.
Aliyasema hayo jana alipokuwa anazungumzia uamuzi wa kuzipeleka fedha hizo Ikulu kama hautakuwa na athari kwenye bajeti ya Bunge hususan kwenye malipo ya posho na mishahara ya wabunge.
Tayari katika baadhi ya mitandao ya kijamii zipo taarifa zinazodai kuwa ofisi ya Bunge imefikia uamuzi wa kupeleka mabilioni hayo ya fedha Ikulu wakati baadhi ya wabunge wakiwa hawajalipwa posho zao na Bunge lenyewe likiwa linakabiliwa na ukata.
Akizungumzia taarifa hizo, Dk Kashilillah alisema ni taarifa potofu kwa sababu fedha zilizowasilishwa kwa Rais Magufuli ni zile ambazo hazikutumiwa na Bunge kati ya Julai na Oktoba mwaka jana, baada ya kuvunjwa kupisha uchaguzi mkuu.
“Huwa ninapata shida kuzungumzia mambo ya kuokota okota, tulipokuwa tunamkabidhi Rais hizo fedha tulieleza na kama kuna mtu anataka taarifa anapaswa kuuliza mamlaka husika siyo kusambaza uongo.
Ni kweli kwamba tumejibana sana kuokoa fedha hizo lakini pamoja na kujibana huko hizi fedha ni za Bunge la 10 ambalo halikufanya kazi kati ya Julai hadi Oktoba mwaka jana.
“Jumla ya fedha tulizookoa ni Sh bilioni 20, lakini sehemu nyingine za fedha hizo tulitumia kulipa gharama za wabunge wapya kama unavyojua idadi ya wabunge sasa imeongezeka pamoja na shughuli nyingine za Bunge. Zilizobaki zilikuwa lazima zirudi, ndiyo utaratibu ulivyo,” alisema Dk Kashalillah.